LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 28, 2018

DK. BASHIRU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA HONG KONG

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally  akizungumza na mwakilishi wa heshima wa Tanzania Hong Kong na Macao nchini China Annie Suk Ching Wu, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Dk. Bashiru na mgeni wake wamejadili kuhusu  ufunguzi wa fursa mpya za kuwasaidia  watanzania kujisimamia kiuchumi, kufungua Miradi ya Ujasilia Mali, fursa za Masomo barani Asia, pamoja na nafasi za ajira na hususan katika kundi la vijana na wanawake.

Katibu  Mkuu aliambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu anaeshuulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ndugu Ngemela Lubinga, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mama Gaudensia Kabaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Tanzania ndugu Erasto Sima na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) ndugu Raymond Mangwaya.

Annie Suk Ching Wu amesema ni wakati muafaka sasa kwa CCM  kuwaandaa vijana wa Tanzania wenye nia na uwezo wa kuwa viongozi wa baadae kwa kuwajengea uwezo na maarifa ili waje kuwa Viongozi wazuri wenye manufaa katika nchi hapo baadae hivyo ameahidi kutoa nafasi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu  na programu za kufundisha  masuala ya Uongozi kwa Vijana na Wanawake kama sehemu ya mchango wake kwa Tanzania.

Akihitimisha Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru  pamoja na kumshukuru Wu amesema CCM na Serikali zake ziko katika ukombozi wa kiuchumi baada ya kujikomboa kisiasa na kuwa Chama kinalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida anufaike na uchumi hivyo Chama na Serikali vina mpango wa kuimarisha uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuanzisha  Viwanda sambamba na kutafuta masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi  hivyo ujio wa Mwakilishi huyo ni fursa ya kipekee kwa watanzania.

Matukio yanayoendelea sasa ya Chama kutafuta fursa na wadau wa kimataifa ni sehemu ya Chama kujiimarisha katika nyanja za kiuchumi na kidiplomasia kama njia ya kutekeleza dhana ya    mageuzi ya kukirudisha Chama kwa wanachama katika  wakati huu wa CCM mpya Tanzania mpya.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages