LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 2, 2018

ZARIF AMFAHAMISHA TRUP KUWA HATAFANIKIWA KWA VITISHO, VIKWAZO NA PROPAGANDA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumjibu rais Donald Trump wa Marekani aliyedai kuwa yuko tayari kukutana na wakuu wa Iran.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Zarif  amesisitiza kuwa vitisho, vikwazo na harakati za kipropaganda hazitakuwa na manufaa yoyote na kuongeza kuwa, Marekani inapaswa kujilaumu yenyewe kwa kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA.
Zarif amesistiza kuwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA yalifikiwa kutokana na jitihada za mazungumzo ya wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani na Umoja wa Ulaya na kuongeza kuwa mpatano hayo yalikuwa ya kipekee ya kimataifa na yalikuwa yanaendelea vizuri.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewanasihi pia Wamarekani kuwa wanapaswa kuheshimu taifa la Iran na mikataba ya kimataifa.
Trump
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Jumatatu akiwa ameandamana na Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte, Trump alijibu swali kuhusu uwezekano wa kufanya mazungumzo na Iran na kudai kuwa: 'Wakati wowote ule' na 'bila masharti yoyote' niko tayari kufanya mazungumzo na wakuu wa Iran.'
Rais wa Marekani anahadaa umma kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hali ambayo Mei nane, kwa kukariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran alitangaza kuondoka nchi yake katika mapatnao ya nyuklia ya JCPOA na kurejesha vikwazo vipya. Hatua hiyo ya Trump ya kujiondoa katika mapatnao ya nyuklia ya Iran ililaaniwa vikali kimataifa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages