Wasichana wametakiwa kujipanga 'kuvaa
magauni manne' ili kuhakikisha ndoto zao za maisha zinakamilika ambapo magauni hayo yametaajwa kuwa ni ni Sare ya Shule, Joho
la Mahafari (Graduation), Gauni
la Harusi na Gauni la Ujauzito ambalo ni la nne.
Hayo ni katika baadhi ya yaliyosemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mwanshinga
Mlozi (PICHANI), wakati akizungumza na Waanadishi wa Habari jana, katika Ukumbu wa Kamati Kuu, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILIMI
MKUTANO WA VYOMBO VYA HABARI NA KATIBU MKUU WA UWT TAIFA KITAKACHOFANYIKA UKUMBI WA KAMATI KUU OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA
TAREHE 23/08/2018
1.0
UTANGULIZI
Naomba
kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia Afya njema, aidha
nichukue fursa hii kuwakaribisha watanzania wote wanawake kwa wanaume kuja
kunisikiliza nikizungumza kuhusu masuala ya Umoja wa Wanawake Tanzania .
2.0
PONGEZI KWA MHESHIMIWA DKT. JOHN
POMBE MAGUFULI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MWENYEKITI WA CHAMA CHA
MAPINDUZI TAIFA)
i)
Pongezi kwa mwenyekiti wa UWT Taifa
ii)
Uteuzi wangu.
iii)
Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya
Uchaguzi (2015 – 2020).(ambao
ndio mkataba wetu na wananchi
Sekta za huduma za
Kijamii zinazomgusa mwanamke. (ilani
sura ya nne uk 81-109 inaeleza kuwa hizi
ni nyenzo muhimu katika kuondoa umaskini na kuharakisha maendeleo ya wananchi.)
(a)
Sekta ya Afya.
Kwa muda mfupi takribani miaka miwili
na nusu tumeona ongezeko la bajeti na ujenzi wa Vituo vya Afya 260. Vituo hivi
vina hadhi ya Hospital kila kituo kimepewa jumla ya Tshs. 700,000,000/= Milioni
500,000,000/= kwa ajili ya ujenzi na Tshs. 200,000,000/= kwa ajili ya vifaa vya
Tiba. Nina imani vituo hivi vitapunguza vifo vya mama na mtoto
(b)
Sekta ya Elimu.
-
Elimu bure kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na
Sekondari.
-
Ongezeko la mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Bilioni 80 hadi takribani Bilioni
500. Hivyo, wasichana tunawahimiza kusoma kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi). Mfano, kuwasisitiza watoto wakike
kutokupata mimba/ndoa za utotoni.
Wasichana Wanatakiwa kujipanga kuvaa
magauni manne:
-Gauni la
kwanza: Sare ya Shule.
-Gauni la pili: Joho
la Mahafari (Graduation)
-Gauni la tatu: Gauni
la Harusi.
-Gauni la nne: Gauni la Ujauzito.
Wasichana wanaharibu
ndoto yao kwa kuanza kuvaa gauni la nne bila kufuata mpangilio
c) Elimu
ya Ufundi Stadi
Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi imeamua kufanya majaribio kutoa mafunzo kwa Vijana hasa ya
kujiunga na Mafunzo ya VETA ambayo yatakuwa
ni bure. Hii ni utekelezaji wa kupunguza tatizo la Ajira kwa Vijana
sambamba na kumwandaa katika kujiajiri. Hii ni fursa ya pekee kwa watoto
wakike.
d) Sekta ya Maji.
Bajeti ya Sekta ya Maji imeongezeka
ikiwa ni sambamba na kuanzisha miradi mikubwa ya maji katika maeneo mbalimbali
Nchini. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Kampeni 2015 alitoa ahadi ya kumtua Mwanamke Ndoo kichwani. (zaidi
ya billion 700 zimekwishatolewa na takribani trillion 1.7 kwa miaka mitatu ijayo zimepangwa kutolewa)
Pamoja na hayo Umoja wa Wanawake wa
Tanzania (UWT) kwa kuzingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na Katiba ya UWT
inazungumzia juu ya kumkomboa Mwanamke:
-
Kiuchumi
-
Kijamii
-
Kisiasa
3.0 VIPAUMBELE VYA UMOJA WA WANAWAKE WA
TANZANIA (UWT) (2018/2019)
7.1 Kwa
kuzingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na Katiba ya UWT tumeandaa Mpango kazi
ambao vipaumbele vipo 18 (2018 – 2022) kwa mwaka wa kwanza (2018 – 2020) tuna
vipaumbele vifuatavyo:-
i)
Kusimamia na kufuatilia Utekelezaji
wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2018 – 2020) hasa katika huduma za Jamii
-Maji
-Elimu
-Afya
Mama na Mtoto
ii) Kujiimarisha
Kiuchumi, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha vilivyopo kuanzia ngazi
ya Kata, Taifa. Sambamba na kubainisha mali zote za UWT.
iii) Kuongeza
Idadi ya wanachama kuanzia ngazi ya Tawi hali Taifa, kwani wanawake ni Mtaji
hasa nyakati za Uchaguzi.
iv) Kuwajengea
uwezo Viongozi, Watendaji wanachama na Vikundi vya wanawake vya Kiuchumi na
Kijamii.
Ninawapongeza
viongozi wa UWT (kamati za utekelezaji) ngazi ya mkoa na wilaya kwa kusimamia
na kufuatilia utekelezaji wa ilani, wanafanya kazi nzuri ninawaomba kutuma
taarifa makao makuu kwa ajili ya kumbukumbu
4.0
MAFANIKIO YA UWT
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)
imeendelea kuwaletea wanawake mafanikio mbalimbali katika Nyanja tofauti kama
ifuatavyo:-
i)
Imeweza kuunganisha wanawake na
kuwaletea mshikamano.
ii)
Kupigania haki za wanawake kwa usawa
yaani 50 – 50 ambapo mpaka sasa tumefikia asilimia zaidi ya 36 na bado
tunaendelea.
iii)
Kuwajengea uwezo, kuelimisha Jamii na
kukemea uonevu wa kijinsia na kuweza kupata Dawati la Kijinsia kuendelea kuwa
kimbilio la wanawake.
Pia ofisi ya UWT ina
dawati maalum la kushughulikia malalamiko/kero zinazowasibu wanawake
Ninawapongeza
Viongozi wenzangu wote waliofanikisha katika kukisukuma Chombo hiki cha
Wanawake ambacho ni tegemeo kubwa la Chama Cha Mapinduzi na wanawake kwa
ujumla. Nani Kama Mama Hakuna. Mama
ni Mlezi wa Familia, Mlezi wa Jamii, Mlezi wa Taifa. Nami ninaahidi kutumia
uwezo wangu wote, nguvu zangu zote, ujuzi wangu wote na elimu niliyoipata
katika kuwatumikia wanawake. Ninaomba wanitume mimi ni mtumishi wenu.
5.0 UWEZESHAJI WA WANAWAKE KIUCHUMI
Katika
Ilani ya Uchaguzi Sura ya 5 Ukurasa 117 Ibara ya 61 inazungumzia Uwezeshaji wa
wanawake Kiuchumi. Halmashauri nchini kwa kutumia mapato yao ya ndani
yameelekezwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kutenga (4%) kwa ajili ya mikopo ya wanawake sambamba na Vijana (4%) na watu
wenye Ulemavu (2%), kuwapatia mikopo
hiyo bila Riba.
Tamko
la Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa maelekezo kwamba fedha
hizi zitolewe bila ubaguzi wa rangi,ubaguzi wa dini,ubaguzi wa itikadi, urasimu
na manyanyaso ili kila mwanamke wa Tanzania aweze kupata hasa katika kuinua
Uchumi wa familia na Taifa. Fedha hizi
pia hazitakuwa na marejesho yenye riba.
Tunawasisitiza
Makatibu wa UWT wa Wilaya kusimamia na kufuatilia mgao wa fedha hizo uendelee
kuwa wa haki kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilaya.
Tunawapongeza Viongozi wa Chama na
Serikali kwa kusimamia na kufuatilia kutekeleza Ilani. Halmashauri ambazo
hazitengi fedha hizo, Viongozi wafuatilie kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi.
6.0 UTEUZI
WA WANAWAKE KATIKA NAFASI MBALIMBALI
Tunaendelea kumshukuru na kumpongeza
kwa Moyo wa dhati Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wetu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwateua wanawake na hasa vijana wa kike katika nafasi
mbalimbali za juu za Maamuzi.
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)
umesikitishwa sana na baadhi ya Kauli
zilizotolewa za kudhoofisha uteuzi wa wanawake hasa vijana wa kike.
Tunamwomba Mhe. Rais asikatishwe tamaa
aendelee kutuamini na kututeua katika nafasi mbalimbali za uongozi kama
anavyoendelea kufanya sasa. Wanawake kwa umoja na mshikamano tuungane kukemea
kauli hizo.
7.0 UCHAGUZI WA MAJIMBO NA KATA
Tangu awamu ya Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi zimefanyika chaguzi kadhaa za
marudio za Majimbo 6 ya Kinondoni, Siha, Longido, Buyungu, Singida kaskazini na
Songea Mjini na Kata 141. Chaguzi hizi zilifanyika kikatiba, na
Chama Cha Mapinduzi kimeibuka kidedea katika chaguzi zote hizo.
Mfano:
Januari
2017 – ushindi Kata 21
Januari
2018 – ushindi Kata 43
Agosti
2018 -
ushindi Kata 77
Tunawapongeza wanawake wote wa CCM,
UWT na wanawake wengine kwa kuhakikisha ushindi wa kishindo unapatikana. Umoja
wa Wanawake wa Tanzania (UWT) inalaani vitendo vya vitisho vinavyotolewa kwa
wanawake na baadhi ya Vyama vya Siasa ili wanawake wasitoke kupiga kura.
Jambo hili tumelifuatilia na kuwaomba
wanawake tuendelee kupambana kwa nguvu zetu zote kwani tangu Uhuru wanawake
walikuwa wapambanaji katika kuikomboa nchi yetu kutoka kwa Wakoloni. UMOJA NI USHINDI.
Tunaiomba Serikali yetu sikivu ya Chama
Cha Mapinduzi, inayoongozwa na Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli ihakikishe inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya Ulinzi
na Usalama hasa wakati wa Uchaguzi sambamba na nyanja zingine kwa lengo la
kuwalinda wanawake na watoto
MWISHO
Wanawake
tuendelee kuchapa kazi na kuhakikisha tunaakisi kauli za Mhe.Rais wetu ya HAPA KAZI TU. Umoja wa wanawake
unategemea kuona wanawake wanawajibika kila mtu kwa nafasi yake aidha wanawake
tuna mchango mkubwa wa kuhakikisha Tanzania ya viwanda inayopelekea uchumi wa
kati.
Asanteni
sana kwa kunisikiliza.
Nawashukuru
wote kwa ujio wenu, Mungu awabariki
WANAWAKE NI JESHI KUBWA
TUJITAMBUE NA KUJITHAMINI
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzani.
Mungu Ibariki UWT.
CCM MPYA, TANZANIA MPYA
CCM MPYA , UWT MPYA
KIDUMU CHAMA CHA
MAPINDUZI
………………….
Mwl. Queen Mwanshinga
Mlozi
Katibu Mkuu wa
UWT-Taifa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇