: Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Cliford Tandari akiteta jambo na wajumbe Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) pamoja na watendaji wa mpango huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Daniel Ole Njolay (katikati) walipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro hivi karibuni. Kutoka kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Emmanuel Mayeji, Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe, Mwenyekiti mstaafu wa kamati hiyo Kapteni John Chiligati na mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Ibrahim Janabi.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Wanawake Wazalishaji wa Chakula Tanzania (WFPT), Bibi. Emmy Kiula hivi karibuni mjini Morogoro. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akikagua kifungashio cha mvinyo
Mwenyekit
wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akiongoza kikao cha
majumuisho baada ya kuhitimisha ziara ya siku 12 kukagua maendeleo ya
utekelezaji ya shughuli za Urasimishaji Ardhi na Biashara katika maeneo ya
Urambo, Bariadi, Ikungi, Chamwino na Manispaa ya Morogoro kikoao kilichofanyika
mjini Morogoro mapema hivi karibuni. (Picha
na: Frank Shija- MAELEZO)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇