|
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu Bi. Rehema Mashinje (mwenye fulana ya mistari), akiungana na wafanyakazi wa Shirika hilo kusherehekea ushindi wa kwanza (kipengele cha mashirika ya serikali), kwakuwa banda bora kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane mwaka 2018 yaliyoadhimishwa kitaifa Mkoani Simiyu Agosti 8, 2018.
NA
SAMIA CHANDE, SIMIYU
SHIRIKA
LA UMEME NCHINI, (TANESCO), limeibuka
mshindi wa kwanza katika kipengele cha Mashirika ya Serikali kwenye maonesho ya
wakulima ( NANE NANE) katika
viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ambapo kauli mbiu ya mwaka 2018 ni “Wekeza
katika kilimo mifugo na uvuvi kwa
maendeleo ya viwanda”.
Katiaka
maonesho hayo TANESCO iliweza kutoa elimu mbalimbali kuhusu umeme pamoja na
matumizi bora ya umeme.
Meneja
wa TANESCO mkoani Simiyu Bi. Rehema Mashinje alisema katikanmaonyesho haya Nane
Nane TANESCO tumejipanga kutoa huduma
bora na kwa welendi mkubwa.
Pia
alitoa rai kwa kwa mananchi wote kutumia fulisa hii ya nane nane kutembelea
banda la TANESCO ili kupata elimu mbalimbali kuhusu maswala ya umeme
hususani kuhusu miradi ya umeme vijiji(REA) ili kuhakikisha kila wananchi
wote wanaopitiwa na mradi wa Umeme Vijini( REA) wanaonganishwa na huduma hiyo
mara moja.
Aliongezea
kwa kusema bila umeme hamna kitu
kinaweza kuendelea hivyo wananchi walime kwa bidi ilitupate mazao mengi tuweze kuendeleza viwanda vyetu na sisi
TANESCO tumejipanga kuhakikisha viwanda vyote vinapata umeme wa uhakika.
TANESCO
kama mdau muhimu iliweza kuhakikisha mabanda yote katika viwanja vya Nyakabidi
vinapata umeme wa uhakika muda wote.
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba
alifungua rasmi maonyesho katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi
wote wa mikoa inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga Kutumia fursa
ya kutembelea katika maonyesho hayo ili kujifunza mbinu mbalimbali za
kitaalamu katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Katika
kufunga maonyesho raisi Mtahafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa
alisema kua kiwanja hiki cha Nyakabindi
kitumike kama darasa la wakulima, wavuvi na wafugaji.
|
|
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu Bi. Rehema Mashinje pamoja na Mkurugenzi wa REA Bwana Amos Manga wakisherekea Ushindi katika maonyesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi
|
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye banda la TANESCO ili kupatiwa habari mbalimbali zihusuzo huduma zitolewazo na Shirika hilo.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye banda la TANESCO ili kupatiwa habari mbalimbali zihusuzo huduma zitolewazo na Shirika hilo.
Wanafunzi wa Simiyu Golden Open School wakiwa wamekabidhiwa madafutari katika banda la TANESCO bada ya kujibu kwa usahihi maswali kuhusu umeme na matumizi yake.(PICHA NA SAMIA CHANDE)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇