Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake mkubwa, Riek Machar wamehimiza kuheshimiwa kikamilifu mapatano ya mwisho ya kugawana madaraka kwa shabaha ya kukomesha vita vya ndani vya umwagaji mkubwa wa damu vilivyodumu kwa miaka mitano sasa.
Itakumbukwa kuwa mahasimu hao wawili wa Sudan Kusini wametiliana saini makubaliano ambayo kwa mujibu wake, Riek Machar atarejea kwenye serikali ya umoja wa kitaifa akiwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais. Kwa mujibu wa mapatano hayo, serikali ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini itakuwa na makamo watano wa rais.
Mapatano hayo yametiwa saidi mbele ya mataifa wa Sudan, Kenya, Uganda na Djibouti.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo mapya, serikali ya umoja wa kitaifa ya Sudan itakuwa na mawaziri 35 wakiwemo 20 kutoka upande wa Salva Kiir, 9 kutoka kwa Riek Machar na waliobakia kutoka makundi mengine ya waasi.
Sudan Kusini ambayo ni nchi changa zaidi barani Afrika ilitumbukia kwenye machafuko ya ndani tangu mwezi Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu Riek Machar aliyekuwa makamu wake wakati huo kuwa alipanga kumpindua.
Mapigano makali yalizuka baada ya hapo na kuitumbukiza nchi hiyo katika shimo la chuki za kikabila, umwagaji mkubwa wa damu, vitendo vya ubakaji, uporaji na janga kubwa la wakimbizi na maradhi ya kuambukiza.
Hata maafisa wa kimataifa wa kutoa misaada ya kibinadamu hawakusalimika na janga lililosababishwa na ugomvi wa makundi hasimu huko Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇