Kiongozi wa Chuo cha Imam Swadiq (as) jijini Dar es Salaam, Tanzania Sheikh Hemed Jalala, ametoa mwito kwa watu wa dini tofauti kuishi kwa maelewano, amani na utulivu.
Sheikh Jalala amesema kuwa, sababu ya Mwenyezi Mungu kumfanya Nabii Ibrahim (as) ambaye anakubaliwa na watu wa dini zote za mbinguni kuweza kuitangaza ibada ya Hijja, ilikuwa na falsafa ya pana nayo ni uvumilivu na maelewano kati ya watu wenye imani tofauti.
Katika uwanja huo, kiongozi huyo wa Chuo cha Imam Swadiq (as) jijini Dar es Salaam ameongeza kwamba, ili nchi iweze kufikia maendeleo na uchumi bora, kwanza itahitajia jambo muhimu zaidi ambalo ni amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇