Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanakijiji wa Rubambagwe plot (Chato) wakati alipokwenda kutoa pole kwenye msiba wa Patricia Tibengana Mazigo 75 aliyefariki juzi tarehe 16-8-2018 Chato mkoani Geita. Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw Gerson Msigwa, ameandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter kuwa Rais Magufuli amefiwa na dada yake, Bi.Monica Joseph Magufuli, aliyekuwa amelazwa kwenye wodi ya uangalizi maalum (ICU), ya hospitali ya Bugando jijini Mwanza. Bi. Mo nica amefariki ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais kufika hospitalini hapo kumjulia hali. (PICHA NA IKULU)
Katika picha hii ya maktaba iliyopigwa na Ikulu inamuonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Dada yake Monica Joseph Magufuli ambaye amelazwa katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza leo Agosti 18, 2018.
Marehemu Monica Joseph Magufuli, Enzi za uhai wake
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇