LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 23, 2018

NMB YACHANGIA MASHUKA YA WAGONJWA MOI YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 5

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI). Dkt. Respicious Bonifac (wa pili kulia) akikabidhiwa msaada wa shuka na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Muhimbili, Happness Mengi kushoto, wanao shuhudia ni viongozi wa taasisi hiyo. (PICHA ZOTE NA KHMISI MUSSA).



NA KHAMISI MUSSA



Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amepokea msaada wa mashuka wenye thamani ya shilingi milioni 5.
Akizungumza katika hafla ya kupokea mashuka hayo alisema "Tunaushukuru uongozi wa Benki ya  NMB Tawi lililopo Muhimbili kwa ushirikiano wanaotupa na kuona nasi ni sehemu yao, kwa kutusaidia shuka za wagonjwa za kulalia. Bonifac alisema hayo wakati wa makabidhiano katika Taasisi ya Tiba (MOI)" Dkt Boniface



Pia alisema MOI inaishukuru NMB kwa msaada kwani MOI  inawahudumia watanzania wasiokuwa na chochote na wengine na Serikali inatusaidia sana kwa hili, hivyo kwa Taasisi iliomba msaada wa shuka hasasa kwa wagonjwa wetu wasiokuwa na chochote



Tuliomba msaada wa mashuka kwa sababu niwatu wetu wa karibu tunao muda mrefu na hawakusita waksema tutafikiria na leo ndio siku maalumu wanatukabidhi msaada wa mashuka 170 yenye thamani ya Sh. Milioni 5. 



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba wa MOI Dkt Samuel Swaai alisema "Niseme kwa niaba ya wenzangu wa Taasisi ya Mifupa (MOI), tunashukuru sana uongozi wa NMB Tawi la Muhimbili kwa msaada wao na kwaniaba ya Serikali tunashukuru sana Mungu awabariki na mlipotowa Mungu awaongezee mlilolifanya ni kubwa na maaranyingi vitu vya namna hii hupata baraka toka kwa Mungu, kwa kumalizia napenda kusema asanteni sana".

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages