Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-NFRA)
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Na Mathias Canal, NFRA-Simiyu
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo amepongeza Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa elimu wanayoitoa kuhusu njia
bora za kuhifadhi nafaka ya mahindi mara baada ya kuvuna.
Nyongo ametoa pongezi hizo jana 8 Agosti 2018 wakati
akizungumza na uongozi wa NFRA mara baada ya kutembelea banda la NFRA kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe
za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji
wa Bariadi Mkoani Simiyu ambapo Rais mstaafu wa srikali ya awamu ya tatu
Mhe Benjamini Willium Mkapa ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha
maadhimisho hayo.
Pamoja na mambo mengine Mhe Naibu Waziri Nyongo
amepongeza elimu inayotolewa kuhusu utunzaji huo wa mahindi mara baada ya
kuvuna kwa kufuata taratibu zote za kuvuna wakati muafaka, ikiwa ni pamoja na Kukausha
vizuri mahindi baada ya kuvuna.
Mhe Nyongo pia amepongeza elimu inayotolewa na NFRA kuhusu
utambuzi wa mahindi kama yamekauka kwa kutumia njia za kienyeji ambazo ni
rafiki kwa wakulima wa chini pamoja na njia za kisasa.
Pia alijionea na elimu kuhusu matumizi bora ya mifuko ya
kuhifadhia mahindi ikiwa ni pamoja na mifuko ya PICS, Vihenge vya chuma
sambamba na maghala ya tofali.
Alisema kuwa njia hizo zitaleta ufanisi iwapo mahindi
yameandaliwa vizuri kabla ya kuhifadhi huku akiisihi NFRA kuongeza nguvu katika
utoaji elimu ili wakulima waweze kunufaika kwani mkulima akielimika ipasavyo ni
sehemu ya mafanikio ya mtu mmoja mmoja sambamba na ukuzaji wa uchumi wa Taifa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇