Mwanza.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa Bugando, jijini Mwanza, Mtawa Suzan Bathlomeo (Pichani) amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.
Habari zilizomkariri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana akithibitisha kutokea kwa tukio hilo zimesema kuwa taarifa kamili zitatolewa na Polisi kwa Kamanda huyo kuzungumza na waandishi wa habari baadaye.
Kwa mjibu wa ofisa uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele Mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumziwa suala hilo na kutaka litafutwe shirika la watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba mkoani Kagera.
“Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala hilo,” amesema Lucy.
Your Ad Spot
Aug 28, 2018
Home
Unlabelled
MTAWA AFARIKI KWA KUJIRUSHA TOKA GHOROFANI JIJINI MWANZA, ALIKUWA MKURUGENZI WA FEDHA NA MIPANGO HOSPITALI YA BUGANDO
MTAWA AFARIKI KWA KUJIRUSHA TOKA GHOROFANI JIJINI MWANZA, ALIKUWA MKURUGENZI WA FEDHA NA MIPANGO HOSPITALI YA BUGANDO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇