Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu waliojificha kwenye mashamba na majumbani.
Alitoa agizo hilo jana Jumatatu Agosti 6, 2018 wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya ya Kasulu na Buhigwe ambapo alisema wahamiaji haramu mkoani humo wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wahukumiwe kifungo.
Kaitka hatua nyingine RC Maganga alioomba mahakama kuhakikisha kesi zote za wahamiaji haramu zinapewa kipaumbele ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani, ambao wanakula chakula bila kuzalisha.
Alisema kuna wahamiaji haramu na wakimbizi waliotoroka kambini wanaishi mitaani na kwenye nyumba za wananchi kinyume cha sheria, jambo ambalo halikubaliki.MKUU WA MKOA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇