LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 5, 2018

MBUNGE: RWEIKAZA DONGE NONO KWA WAHITIMU WA DARASA LA SABA

 Mkurugenzi wa Shule ya ST. Anne Marie Academy, Mwenyekiti na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bukoba Vijijini, Dokt. Jasson Rweikiza akizungumza wakati wa Mahafali ya 16 ya Shule ya Awali na 15 ya Darasa la Saba.

NA KHAMISI MUSSA


Nitawapa donge nono wahitimu wa darasa la Saba Ninahakika kwa asilimia 100 vijana hawa wameandaliwa vizuri na pamoja na kufanya mahafali haya bado nitawaita wazazi kusherehekea ushindi wa vijana wenu. 


Hayo aliyasema wakati wa Mahafali ya 16 Shule ya Awali na 15 Shule ya Msingi Darasa la saba, ambapo anahitaji wafurahiye ushindi wao pamoja na wazazi wao kwani mmesikia ufaulu mwaka jana ulikuwa mzuri sana.


Pia nipende kuwashukuru wazazi kwa ushirikiano wao na waalimu na kujitahidi kulipa ada kwa wakati, binafsi ninafurahiya kuona wazazi wanavyo jitahidi kulipa ada kwa wakati.

Ndugu wazazi wageni waalikwa nami niungane na waliotangulia kusema kabla yangu kwa kuwakaribisha katika shule yetu hii kubwa maridhawa katika Mahafali tukiwa na furaha ya kusherehekea mahafali yetu

Kinacho nifurahisha ni watoto wetu wameiva na ninauhakika wa asilimia 100 vijana hawa kwa sababu wameandaliwa vizuri na watafaulu, lakini pamoja na hayo nitawaita wazazi kusherehekea ushindi.

Napenda kutoa ahadi ya Donge nono kwa wahitimu wa darasa la saba endapo kama watafaulu vizuri ili wafurahie ushindi wao na ninatoa ahadi hii mbele ya wazazi nitawazawadia na mwisho nipende kwashukuru waalimu wote kwa kuwa timu moja asanteni sana.


Mkurugenzi wa Shule ya ST. Anne Marie Academy, Mwenyekiti na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bukoba Vijijini, Dokt. Jasson Rweikiza akipata maelezo mafupi wakati alipotembelea moja ya banda la zimamoto kutoka kwa mwanafunzi wa Kidacho cha Pili, Kathrin Mujungi (wa kwanza kushoto) kabla ya Mahafali ya 16 Shule ya Awali na 15 Shule ya Msingi  
Mkurugenzi wa Shule ya ST. Anne Marie Academy, Mwenyekiti na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bukoba Vijijini, Dokt. Jasson Rweikiza (mwenye koti jeusi) akifuatilia jambo
Askari wa Zimamoto wa Shule hiyo, Bahati Salumoni akizima moto kwa majaribio mbele wa mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi Bukoba Vijijini, na  Mkurugenzi wa Shule ya ST. Anne Marie Academy (pichani hayupo)


































Mwalimu wa Shule ya ST. Anne Marie Academy, Denis Ndulu (kulia) akikabidhiwa zawadi na mzazi wa  Eunice Bulula na Gabriela Bulula, Mary Kalinga ambaye ni Muuguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI, katika ni mwalimu wa shule ya Awali wa shule hiyo, Bahati Tarimo
Pichani ni wahitimu wa Shule ya Awali ya ST. Anne Marie Academy,  Eunice Bulula kushoto na Gabriela Bulula




 Eunice Bulula kushoto na Gabriela Bulula wakijiandaa kukata Keki mara baada ya Mahafali yao
Kiongozi wa Shule ya Awali ST. Anne Marie Academy, Stella Mtafungwa akilishwa kipande cha keki na wanafunzi wake, Eunice Bulula (kushoto) na Gabriela Bulula katikati
Mkuu wa Shule ya  ST. Anne Marie Academy, Gradius Ndyetabula (kulia) akilishwa kipande cha keki na Eunice Bululla baada ya hafla yao ya Mahafali ya 16 na ya 15 Darasa la Saba yaliyofanyia shuleni hapo 


mwalimu wa shule ya Awali wa shule hiyo, Bahati Tarimo akilishwa Keki na wanafunzi wake,  Eunice Bulula (kushoto) na Gabriela Bulula




Muuguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI, akimkabidhi zawadi yake ya UA Eunice Bulula  










(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages