Maafisa wa afya nchini Yemen wamesema muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umefanya mashambulizi ya anga katika mji wa bandari Hodeida unaoshikiliwa na waasi. Watu 28 wameripotiwa kuuawa na 70 kujeruhiwa. Muungano huo, hata hivyo, umekana kuhusika na mashambulizi hayo. Msemaji wa muungano huo, Kanali Turki al-Malki, amesema hawakufanya mashambulizi yoyote katika mji wa Hodeida na badala yake amewalaumu waasi wa Kihouthi, akiongeza kwamba muungano huo unaendesha mikakati yake kulingana na sheria za kimataifa. Kituo cha televisheni cha Al Misrah kinachoendeshwa na waasi kimeripoti kuwa katika mashambulizi hayo ya jana, watu 52 waliuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa. Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Martin Griffiths, ambaye alizikutanisha pande zote mbili kwa mazungumzo wiki za hivi karibuni ili kuzuia mashambulizi katika mji huo, ametangaza mipango yake ya kuzialika tena mjini Geneva, Uswisi, mnamo Septemba 6, kwa duru ya kwanza ya mazungumzo.
Your Ad Spot
Aug 3, 2018
Home
Unlabelled
MASHAMBULIZI YEMEN YAUA WATU 28 MJINI HODEIDA
MASHAMBULIZI YEMEN YAUA WATU 28 MJINI HODEIDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇