LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 14, 2018

MAMA MZAZI AMUUA MTOTO WA MIAKA 11 NA MWINGINE KUMUWEKEA MWIKO SEHEMU ZA SIRI

Wanawake wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma mbalimbali akiwamo mmoja aliyemuua mtoto wake wa kiume wa miaka 11 kwa kumpiga fimbo kichwani.

Katika tukio jingine mwanamke mwingine anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumsokomeza mwiko sehemu za siri mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka sita.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema hayo leo Agosti 14, 2018 wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya mkoa humo kwa waandishi wa habari.

Kamanda Mutafungwa amesema matukio yote yametokea katika wilaya za Gairo na Manispaa ya Morogoro na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara moja.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages