Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu yenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwemo majaji wateule na Watu ambao wameapishwa leo Agosti 27, 2018 jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kuapishwa kwa majaji wapya watatu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore mara baada ya kuapishwa kwa Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha.
Majaji watatu wapya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu wakiwa wameketi pamoja muda mfupi kabla ya kuapishwa, kutoka kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria) na Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha mpya na Majaji wateule wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao wameapishwa leo mjini Arusha kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania) na kulia ni Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria).(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇