LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2018

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WORLD METEOROLOGICAL ORGANISATION – WMO) PROF. PETTERI TAALAS ATEMBELEA OFISI ZA TMA DAR

  NA MHT

SHIRIKA la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini.

Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA katika juhudi zake  za utekelezaji  wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa

Nae mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru Prof. Taalas kwa uamuzi wake wakutembelea Tanzania na alimuahidi kuwa Tanzania kupitia TMA itaendelea kutekeleza makubaliano yote ya kimataifa yahusuo huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa program za WMO

Ikumbukwe kuwa WMO huratibu na kusaidia katika kuboresha huduma za hali ya hewa katika nchi kama vile kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuweka miongozo inayosaidia utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa viwango na ubora wa kimataifa n.k

Kupitia WMO Tanzania na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imenufaika na kuongezewa uwezo kupitia mafunzo, miundombinu ya hali ya hewa, hushiriki kikamilifu katika shughuli za jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali ya hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change - IPCC). Pia, kushiriki katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera (United Nations Framework for Climate Change Conference - UNFCCC) ambapo mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika makubaliano ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji kimataifa na kitaifa kwa faida ya nchi yetu. 

   Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.
  Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo ya namna ya kuwaandikisha wakulima katika mfumo wa utoajia taarifa za hali ya hewa kilimo kupitia simu za mkononi uitwao FARMSMS kutoka kwa meneja wa huduma za matumizi ya taarifa za hali ya hewa Bw, Isack Yonah

 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo kuhusiana na studio ya TMA inayohusika katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo kuhusiana na studio ya TMA inayohusika katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA Bw. Chuki Sangalugembe kuhusiana na mtambo mkubwa wa kompyuta (Computer Cluster)  

  Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akishuhudia na kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa nchi za Afrika mashariki zilizoko katika Bonde la Ziwa Victoria.

Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas katika picha ya pamoja na menejimenti ya TMA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages