LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2018

KATIBU MKUU UVCCM AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA PILI LA UVCCM MKOA WA PWANI

NA ELISA SHUNDA, KIBAHA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala amezindua mkutano wa Baraza Kuu la Pili la UVCCM Mkoa wa Pwani.

Wakati wa Ufunguzi wa Baraza hilo Katibu Mwangwala amewasihi vijana wa UVCCM Nchini kwenda sawa Kulingana na Dunia jinsi inavyobadilika katika kujenga hoja kwenye mitandao ya kijamii tena si kwa kukurupuka bali kujenga hoja Zenye mashiko ambazo zianbatane na mifano hai ya utafiti au waambatanishe na ushahidi kutoka sehemu mbalimbali.

"Mimi ni mmoja kati ya watu wanaotembelea sana kwenye mitandao ya kijamii naona jinsi vijana wenzangu mnavyokuwa mmepiga picha na kutupia katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo na kukisemea chama chetu kwa wale wenzetu wenye kuweza kuandika wanaandika haswa hivyo basi niwasihi na Vijana wengine nao kuendana na wakati watumie mitandao ya kijamii katika kukisemea CCM katika kazi zinazotekelezwa na Rais Dk. John Magufuli katika kutekeleza Ilani ya Chama na mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ambayo kiuhalisia yanayonekana kwa macho Kijana wa UVCCM tembea kifua mbele" Alisema Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mwangwala.

Amewataka Vijana katika kujenga hoja zao watumie mifano hai ambayo ipo katika mitandao sio wavae nguo za chama na kupiga picha tu watumie nafasi hiyo kusema mambo mema yaliyofanywa na chama chao.

Hata hivyo Katibu UVCCM Taifa Mwangala amewataka makatibu watendaji wote kutekeleza kwa vitendo miradi wanayoiandikia kwenye muswada yao kwa kuwa yeye ni mfuatiliaji asiyetaka kusoma taarifa bila kuona uhalisia wa kilichozungumzwa.

"Naagiza jkwa makatibu watendaji wa mikoa na Wilaya kuzingatia sana na kutekeleza kwa vitendo miradi wanayoiandika kwenye miswada yao Mimi ni mfuatiliaji mzuri tu nisiyetaka kusoma taarifa ya Ndani ya kikao bila kuona kwa uhalisia kile mlichokiandika kama ukiniambia mmeanzisha mradi wa ufugaji wa samaki au Kuku nataka niende nikaone kwa macho yangu mradi huo Sipendi ubabaishaji katika utendaji kazi wangu tuwe makini na Hili" Alisema Katibu Mkuu UVCCM Taifa,Mwalimu Mwangwala.

Akizungumza kwa niaba ya watu wote waliokuwepo kwenye mkutano huo Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Makwiro wameahidi kutekeleza agizo hilo.

Naye Katibu Wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhani Kapeto amemuakikishia Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala kufuata maagizo aliyoyatoa kwa vitendo na kumuahidi matokeo chanya kwa mkoa huo wa Pwani na kumuahidi kutomuangusha katika utendaji wa kazi ndani ya umoja huo wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.
Cont:0719-976633
Email:elisashundaGmail.com

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages