LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 11, 2018

JULIUS MTATIRO AIKIMBIA CUF NA KUJISALIMISHA CCM, LEO



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro (pichani) amejivua uanachama wa chama hicho nakujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Amesema sasa anaona kuwa umewadia ni wakati wake wa kwenda kutumia vipaji vyake kikamilifu pia kuwa balozi mkubwa wa Rais Dk. John Magufuli ndani na nje ya nchi.

Akitangaza uamuzi huo  jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Agosti 11, 2018 Mtatiro amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyia nchi yake maendeleo. 

"Nimeamua kwa dhati kuanzia hivi sasa, kuwa mmoja wa mabalozi wakubwa wa Taifa langu na balozi mkubwa wa Rais wa Taifa hili, na kazi hiyo ntaifanya ndani na nje ya nchi na ntafanya hivyo kwa vitendo na maneno na wala sitasita" - Mtatiro.

"Nimejiridhisha kwa hitaji la Nafsi yangu kwamba nijiunge na Chama cha Mapinduzi CCM, nawajulisha watanzania rasmi kuwa nimeanza mipango ya kutekeleza hili mara moja", -Mtatiro.

"Siendi CCM kutafuta nafasi na ukuu, uamuzi niliofanya ni uamuzi wa kutafuta jukwaa sahihi lakufanya siasa katika kipindi cha mbele cha maisha yangu", amesema Julius Mtatiro na kuongeza;

"Masuala ya misimamo yangu ya sera na ilani za CUF na misimamo ya CUF hayo yanabakia CUF, hivi sasa mimi ni Mtatiro ambaye ninajiandaa kujiunga na Chama cha mapinduzi CCM kama mwananchi nikitumia haki yangu kikatiba".

"Mimi sasa siyo mwanachama wa CUF tena nimejivua nyadhifa zangu zote, sasa naanza kutumia uwezo wangu wote Nitaanza kufanya siasa za vitendo kwa kumshauri Rais kujenga nchi yangu",

"Kuna vijana wadogo tu wamefanya mambo makubwa kwa kuwa wako katika majukwaa sahihi nimetafakari Sana nimeona niachane na siasa za ubabaishaji siasa za ushabiki" -Julius Mtatiro.

Amesema ameshamwandikia Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, kuhusu msimo wake kuhusu kuachana na Chama hicho, na sasa amefanya maamuzi ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages