LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 3, 2018

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAAHIDI KUENDELEA KUISIMAMIA SERIKALI IPASAVYO KATIKA KUHAKIKISHA MASLAHI YA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO NA SERIKALI YANALINDWA

02 August 2018
Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amekutana na viongozi wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Kariakoo, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam na kufanyanao kikao cha kazi, kwa lengo la kusikiliza kero zao, changamoto zinazowakabili na mashauriano ya fursa mbalimbali ikitafsiri muendelezo wa Chama kushughulika na shida za watu kwa vitendo.

Akizungumza na viongozi hao wa wafanyabiashara wadogo wadogo almaarufu kama machinga Ndg. Polepole amesema CCM ipo tayari kushirikiana, kushauriana na kusaidia makundi mbali mbali ya kijamii katika kuhakikisha ustawi wa makundi hayo na msimamo wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  upo dhabiti katika kuhakikisha  changamoto za wananchi zinapatiwa majibu.

"Ndg. Magufuli anawapenda sana wafanyabiashara, anapenda haki yenu ipatikane na haki ya Serikali pia ipatikane aidha kwa kulipa kodi ama tozo kwa mujibu wa sharia ili Serikali iendelee kuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi" amesema Ndg. Polepole.

Kikao hiki cha kazi kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Kariakoo na CCM kitakuwa na muendelezo hivi karibu ambapo Chama kimesisitiza kuwakutanisha wafanyabiashara hao na wadau na mamlaka zote za Serikali zinazohusika na biashara ili kufanikisha utatuzi wa changamoto zao  kwa kasi na uhakika.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) - OFISI NDOGO MAKAO MAKUU LUMUMBA.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages