LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2018

ZARIF AJIBU BWABWAJA ZA TRUM, AMWAMBIA: KAA CHONJO!

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana usiku alijibu mashambulizi ya maneno ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Dakta Muhammad Javad Zarif amesema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba vitisho vilivyotolewa na Donald Trump havina umuhimu wowote kwa taifa la Iran na kwamba Wairani wamekuwa wakisikia maneno kama hayo kwa kipindi cha miaka 40 sasa. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemwambia Trump kwamba: "Wairani wamekuwepo kwa maelfu ya miaka na wameshuhudia kuporomoka kwa falme na tawala mbalimbali ukiwemo ufalme wao wenyewe uliokuwa na umri mrefu kuliko umri wa baadhi ya nchi; hivyo basi kaa chonjo!"
Akijibu matamshi ya Rais Hassan Rouhani wa Iran aliyeitaka Marekani "isichezee mkia wa simba", Jumatatu ya jana Donald Trump alisema katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba: Ukitoa tena vitisho dhidi ya Marekani, Iran itashuhudia matokeo mabaya ambayo yameshuhudiwa mara chache sana katika historia."
Rais Donald Trump wa Marekani
Jumapili iliyopita Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa hotuba kali akijibu vitisho vya Trump aliyesema kwamba hataruhusu mafuta ya Iran kuuzwa nje ya nchi na kusema: Iran imekuwa ikilinda njia za baharini za Mashariki ya Kati katika kipindi chote cha historia, hivyo usicheze na mkia wa simba, utajuta kwa sababu jibu la Iran litakuwa kali sana." 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages