Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Bibi Pendo Lilola kwa kujifungua salama mtoto wa kiume katika wodi ya wazazi kwenye Hospitali ya wilaya ya Kasulu Julai 29, 2018. Mheshimiwa Majaliwa aliitembelea Hospitali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Julai 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA OWM, KASULU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa hospitali ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa tuhuma za wizi dawa na vifaa tiba.
Pia Waziri Mkuu ameahidi kuyafunga maduka yote ya dawa yanayodaiwa kununua dawa kutoka kwa watumishi wa hospitali hiyo wasioukkuwa waaminifu na kuziuza kwa wananchi.
Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi leo (Jumatatu, Juni 30, 2018) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.
Amewataja watumishi wanaotuhumiwa kuhusika na wizi huo kuwa ni Mfamasia wa wilaya Bw. Michael Nindi, mtumishi wa maabara Bw. Tilas Mbombwe na Bibi. Venansia Batega ambaye ni muuguzi.
“Watumishi hawa nimewasimamisha kazi kuazia leo hii, ili wapisha uchunguzi wa upetevu wa dawa na vifaa tiba zikiwemo darubini mbili. Hospitali hii inamatatizo makubwa sana ya wizi,”.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kutenga siku tatu katika wiki na kuwafuata wananchi waishio vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Pia Waziri Mkuu amewataka watumishi hao waondoe urasimu wanaouweka kwa lengo la kupokea rushwa na pia wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
“Sitarajii kusikia jambo hilo kwa sababu halina nafasi. Vyombo vinavyosimamia maadili ya utumishi vitimize wajibu wake ili kuwalinda wananchi wasiingizwe katika utoaji rushwa,”.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇