LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2018

VIONGOZI MKOA WA SONGWE WATAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO MIONGONI MWAO

  NA OMR, SONGWE
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan awewataka Viongozi wa mkoa wa Songwe kuwa na ushirikiano baina ya Uongozi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kwa siku 5 mkoani Songwe.
Makamu wa Rais amesema kuwa kuna changamoto ya Utawala bora ndani ya Halmashauri hivyo kuutaka uongozi wa mkoa kutoa mafunzo ya utawala bora katika ngazi ya Halmashauri.
Makamu wa Rais amevutiwa sana na shughuli za ujasiriamali na kuutaka viongozi wa mkoa huo kuwasaidia Wajasiriamali hao.
Makamu wa Rais ameuagiza Uongozi wa mkoa kuanzisha program maalum ya kupima afya wakazi wa mkoa huo huku akiweka msisitizo juu ya elimu ya afya na uzazi wa mpango.
Makamu wa Rais amehimiza sana kutunza mazingira na kupanda miti kwa wingi.
Mara baada ya kikao hicho Makamu wa Rais alielekea mkoani Mbeya ambapo alipokelewa na mamia ya watu katika eneo la Mbalizi.
Makamu wa Rais aliwasalimu wakazi wa Mbalizi na kuwapa pole kwa ajali zinazotokea mara kwa mara kwenye eneo la mteremko Mbalizi.
Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto za miundo mbinu za barabara ambapo bara bara ya mchepuko inajengwa ili kupunguza ajali katika mteremko huo korofi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka wananchi kuendelea kutunza Amani na Utulivu na kuahidi kutekelezwa  kwa ahadi zote zilizotolewa.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Songwe kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Chiku Galawa.
 Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa Mbalizi wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages