LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2018

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILI WAKULIMA WAWEZE KUYAFIKIA MASOKO KWA URAHISI: MAKAMU WA RAIS SAMIA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya barabara hasa za ndani kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

“Serikali imetoa shilingi bilioni 6 kujenga barabara ya Rujewa – Ubaruku inajengwa kwa kiwango cha lami”

Makamu wa Rais ameipongeza kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd kwa kujenga kituo cha afya kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu kumi na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja.

Aidha Makamu wa Rais amesema migogoro yote itafanyiwa kazi kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mmoja.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed  ameahidi kuwalipia deni la shilingi milioni 800 wakulima wanaodaiwa deni waliokupa kununulia power tila

Mbunge huyo wa Mbarali amesema kuwa Serikali ya awamu imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Akizungumza na Wananchi wa Kapanga katika mkutano huo, Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameahidi kutoa mifuko 200 kutoka kwenye Taasisi yake ya Tulia Trust kusaidia ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika kituo cha Kapanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd , kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika kukoboa na kufungasha mpunga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd , kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika kukoboa na kufungasha mpunga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages