Polisi ya Nigeria wametangaza kwamba maafisa usalama wa nchi hiyo wamewatia mbaroni wanachama 22 na viongozi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema kuwa, maafisa usalama wa Nigeria pia wamefanikiwa kuwanasa waratibu zaidi ya 50 wa mashambulio ya kujitoa muhanga katika jimbo hilo ambao akthari yao pia walishiriki katika kuwateka nyara wanafunzi wa shule ya mji wa Chibok. Mwezi Aprili 2014 kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilivamia shule ya mji wa Chibok, na kuwateka nyara wanafunzi wa kike wapatao 276. Tangu ku wakati huo na licha ya kupita miaka miinne sasa, bado hatma ya wanafunzi 100 haijulikani.
Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi yake tangu mwaka 2009 huko kaskazini mwa Nigeria ambapo katika hujuma hizo zaidi ya watu elfu 20 wa nchi hiyo na nchi jirani wameuawa. Aidha zaidi ya watu milioni mbili na laki sita pia wamekuwa wakimbizi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇