Duru za habari zimeripoti kwamba Korea Kaskazini imeanza kubomoa kituo cha kurushia makombora cha Sohae katika mji wa Pyongan.
Kwa mujibu wa habari hiyo, eneo hilo la mashine za makombora, linapatikana katika kituo kikuu cha kurushia satalaiti cha Sohae katika mkoa wa Pyongan, na ambalo tangu mwaka 2012 kilikuwa kituo muhimu kwa ajili ya kurushia makombora na majaribio ya mitambo ya makombora kwa nchi hiyo. Aidha eneo hilo linatajwa kuwa moja ya mafanikio makubwa ya teknolojia huko Korea Kaskazini.
Katika hatua nyingine, Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imetangaza maamuzi ya nchi hiyo kwa ajili ya kupunguza vituo vya ulinzi visivyo vya kiraia katika maeneo ya mpakani pamoja na Korea Kaskazini. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema kuwa, serikali ya Seoul imeazimia kutekeleza suala hilo kupitia fremu ya kuboresha mahusiano ya nchi mbili. Hatua hiyo imeelezwa kuwa inalenga kutambua makubaliano ya kubadili maeneo hayo ya kijeshi na kuwa ya kiraia ikiwa ni hatua ya kuanzisha eneo la amani katika mpaka wa nchi mbili hizo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇