Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa akipongeza uchaguzi wa Bunge nchini Pakistan na kuutaja kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha amani na demokrasia nchini humo.
Stephen Dujaric msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Antonio Guterres ameipongeza Tume ya Uchaguzi ya Pakistan kwa kuendesha uchaguzi huo na kuzingatia mipango mizuri inayohusiana na utoaji elimu na jitihada za kuzidisha ushiriki wa wanawake, vilema na wale wasiojiweza na pia kushiriki wapiga kura kwa mara ya kwanza katika zoezi la uchaguzi.
Dujaric amesema kuwa, Umoja wa Mataifa umeazimia kuendelea kuiunga mkono Tume ya Uchaguzi ya Pakistan na kwamba Katibu Mkuu wa umoja huo anataraji kuwa, serikali mpya ya nchi hiyo itafanikiwa katika kuandaa mazingira ya kudumisha amani, demokrasia na mustakbali mwema wa wananchi wa Pakistan.
Tume ya Uchaguzi ya Pakistan jana ilikitangaza chama cha Tehreek-e-Insaf (PTI) kinachoongozwa na Imran Khan kuwa kimeshinda uchaguzi wa Bunge kwa kupata viti 115 vya uwakilishi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇