LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 17, 2018

IRAN YAWAKAMATA MAGAIDI WENGINE WA DAESH KUSINI MWA NCHI

Maafisa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran wamefanikiwa kuwatia mbaroni wanachama kadhaa wa genge la kigaidi lenye mfungamano na kundi la ukufurishaji la Daesh (ISIS) kusini magharibi mwa nchi.
Mahmoud Alawi, Waziri wa Usalama wa Iran amesema magaidi hao wamekatwa usiku wa kuamkia leo, katika mkoa wa Zanjan, ulioko kusini magharibi mwa nchi, wakipanga njama za kufanya mashambulizi ya kigaidi katika wilaya kadhaa za hapa nchini.
Amesema vyombo vya kiintelijensia vya Iran vimekuwa vikifuatilia nyendo za magaidi hao na hatimaye jana jioni vikafanikiwa kutibua njama zao.
Ameongeza kuwa,  ndugu ya mmoja wa magaidi hao waliokamata aliuawa nchini Syria, na tayari alikuwa ameunda kikundi cha magaidi wanne kwa lengo la kufanya hujuma za kigaidi hapa nchini. 
Mwanachama wa Daesh akitiwa mbaroni na polisi wa Iran
Haya yanajiri chini ya wiki mbili baada ya Abbas Jaafari Dowlatabadi, Mwendesha Mashtaka wa Tehran kutangaza habari ya kutia nguvuni wanaume 16 na wanawake 16 wanachama wa kundi la magaidi wa ISIS ambao walikuwa wamepata mafunzo ya kijeshi nchini Syria.
Magaidi hao walikuwa wamerejea Iran baada ya kundi hilo kushindwa nchini Syria na walikuwa wanapanga njama ya kutekeleza hujuma za kigaidi kabla ya kukamatwa na maafisa wa usalama.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages