Baadhi ya watendaji kutoka Halmashauri za mkoa wa Shinyanga wakisikiliza maelekezo ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kuhitimisha ziara yake alioyoifanya katika Halmashauri za mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuangalia utoajiwa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro akimshukuru Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa ziara yake alioyoifanya katika Halmashauri za mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuangalia utoajiwa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Niabu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiagana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.Rashid Mfaume na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro mara baada ya kuhitimisha ziara yake alioyoifanya katika Halmashauri za mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati mkoani humo.-
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na WAMJW Shinyanga
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kufuata vipaumbele vya Serikali katika maeneo wanayofanya kazi na kutoa huduma .
Ameyasema hayo mkoani Shinyanga wakati akizungumza na wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga wakuu wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Ustawi wa Jamii katika hitimisho la ziara yake mkoani humo.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ni wadau muhimu katika Maendeleo ya taifa ila wanapaswa kufuata vipaumbele vinavyotolewa na Mikoa na Halmashauri wanazoenda kufanya kazi na kutoa huduma.
Ameongeza kuwa katika Mikoa mingi kumekuwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi za aina moja kwa watu wa aina moja hivyo kufanya maeneno mengine kukosa nguvu.

Ametolea mfano changamoto iliyopo ya mimba na ndoa za utotoni katika baadhi ya Mikoa ukiwemo mkoa wa Shinyanga hivyo wadau wanapaswa kuelekeza nguvu katika kupambana na masuala muhimu ya eneo husika.
"Niwapongeze wadau wetu ila pia niwaase tu tuzingatie vipaumbele vya Mikoa na Halmashauri ili kusaidiana na Serikali katika Maendeleo" alisisitiza Dkt. Ndugulile
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa watasimamia kwa kuratibu kwa karibu kazi zote zinazofanywa na wadau.
"Nikuhakikishie Mhe. Naibu Waziri tulisimamia agizo lako kwa ukamilifi" alisema Mhe. Josephine.
MWISHO.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇