Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo imemtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kimara, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, Manota Melikiadi kuwa amepita bila kupingwa.
Akizungumza katika Ofisi ya Kata ya Kimara, Mkurugenzi wa Uchaguzi katika kata hiyo, John Lipesi Kayombo amesema, amemtangaza Manota (pichani), kuwa amepita bila kupingwa kufuatia wagombea watatu wa vyama vingine kukosa sifa za kuteuliwa na Tume hiyo kuwa wagombea kwa mujibu wa sheria.
Kayombo aliwataja wagombea walioenguliwa kutokana na kukosa sifa kuwa ni Monalisa Ndala (ACT-Maendeleo), Josephat Nofola (Chadema) na Abubakar Nyamguma (CUF) na kwamba imebainika hawana sifa baada ya kushindwa kuzitolea utetezi wa kuridhisha hoja za pingamizi walizowekewa na Mgombea wa CCM.
Amesema, kufuatia kuenguliwa kwao wagombea hao wa Chadema, Cuf na ACT Wazalendo wanayo nafasi na kuweza kukata rufani kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndani ya saa 24, vinginevyo Manota tayari ni diwanai wa kata hiyo anayesbubiri kuthibitishwa kwa kupewa cheti chakwe cha ushindi baada ya muda uliowekwa kuanyika uchaguzi kupita.
Akizungumzia hatua hiyo, Manota amesema, licha ya kupita bila kupingwa alikuwa na uhakika wa kuwashinda wenzake hata kama uchaguzi ungefayika kwa kuwa anazo hoja ambazo kwanzo wananchi wangempa kura za ushindi.
"Inasikitikisha kwamba vyama vya upinzani sasa vimekwisha kiasi cha kuweka wagombea wasio na sifa katika uchaguzi muhimu kama huu, bila shaka hii ni dalili ya kufa kwa vyama vya upinzani.
Ila ninachoweza kuahidi hapa ni kwamba mara nitakapoanza kazi baada ya kuapishwa nitawatumikia wana Kimara wote bila kujali itikadi zao", alisema.
Katibu wa CCM Wilaya Ubungo Salum Kally ambaye alifuatana na viongozi kadhaa wa CCM, alisema Chama Cha Mapinduzi kilikuwa kimejipanga vema kuhakikisha mgombea wake anashinda Udiwani na kwamba ushindi ulikuwa ni lazima kwa kuwa CCM ndicho chama kinachokubalika kwa wananchi kuliko vyama vyovyote hapa nchini.
"Tunafurahi kwamba mgombea wetu amepita bila kupingwa, hili ni jambo ambalo linatupa hamasa zaidi ya kuendelea kukiimarisha Chama ili kizindi kupendwa na Watanzania wengi zaidi zaidi." alisema Kally.
Mkurugenzi wa Uchaguzi kata ya Kimara John Kayombo akimtangaza mgombea wa CCM Manota Paschal kupita bila kupingwa
Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kally (kulia) na Mgombea wa CCM Manota Melikiadi wakiongoza kushangilia baada ya Mkurugrnzi wa Uchaguzi Kata ya Kimara kumtangaza mgombea huyo kuita bila kupingwa, leo >Picha na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇