LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 12, 2018

DK. MNDOLWA KUMWAKILISHA DK. MAGUFULI KATIKA MAZISHI YA DIWANI ALIYEFARIKI KWA AJALI MKOANI SIMIYU KATIKA MSAFARA WA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo mjini Bariadi, alipowasili mkoani humo leo kwa ajili ya kumwakilisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwenye mazishi ya Diwani Mahega Masuga selemani wa Kata ya Tindabuligi, ambaye alifariki juzi msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM ulipopata ajali katika eneo la Kisesa Wilayani Meatu mkoani Simiyu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na kulia ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Jumuiya hiyo na Mjumbe wa NEC-CCM Christina Joram na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Simiyu Masunga Yuma.
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania  Haidar haji Abdallah akisalimia wakati wa kikao hicho.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Jumuiya hiyo na Mjumbe wa NEC-CCM Christina Joram akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Simiyu Masunga Yuma akizungumza wakati wa kikao hicho
 Kikao hicho kikiendelea
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa na Makamu wake kwa upande wa Zanzibar haidar Haji Abdallah wakisaini vitabu vya wageni baada ya juwasili ukumbini kufanya kikao hicho.
-TARIME -
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mara na viongozi waliopo katika msafara wake kabla ya kuondoka nyumbani kwa Mjumbe wa NEC, Ndugu Gachuma (watatu kulia) nje kidogo ya mji wa Tarime mkoani humo leo.
"Aina ya mti ule hupatikana kwa wingi sana katika maeneo ya Zanzibar" Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdalla akimuonyesha mti huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi tanzania Dk. Edmund Mndolwa wakati wakiwa nje ya nyumba ya Mjumbe wa NEC Ndugu Gachuma nje kidogo ya mji wa Tarime mkoani Mara.
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah, akiwaeleza sifa za mti huo aina ya Mpweza ambao hupatikana zaidi Kisiwani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mdolwa akiagana na viongozi wa mkoa wa Mara, baada ya kufika katika barabara inayoenda mkoani Simiyu ambako amewasili leo jioni kwa ajili ya kumwakilisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwenye mazishi ya Diwani Mahega Masuga selemani wa Kata ya Tindabuligi, ambaye alifariki juzi, msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM ulipopata ajali katika eneo la Kisesa Wilayani Meatu mkoani Simiyu. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages