LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 26, 2018

WAPUUZENI WANAODAI CCM HAIJAFANYA KITU

Na Augustino Chiwinga
Watanzania wapuuzeni wapinzani wanaodai kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haijafanya maendeleo yoyote , wapinzani hao wanawapotosha na kuwadanganya wananchi hali ya kuwa wananchi wenyewe ni mashahidi wa jinsi nchi inavyopiga hatua ya kimaendeleo siku baada ya siku.

Nashangazwa na watu hao  wanaosema hakuna maendeleo  yoyote yaliyopatikana wakati wanatembea katika barabara za nzuri za lami zilizojengwa na CCM, wanakunywa maji yaliyoletwa na CCM wanatumia nishati ya umeme ulioletwa na CCM na hata wakiumwa wanapata matibabu  kwenye hospital zilizojengwa na CCM.

Siku hizi vijiji vingi vina huduma ya Maji na Umeme wa REA ,Hospitali na Vituo vya Afya  na Zahanati, Mashule kila kona, Wanafunzi wanasoma bure , Mikopo ya Elimu ya
Juu inatolewa, Viwanda vinajengwa, Vijana na Wanawake wanakopeshwa fedha na Serikali ya CCM,  Wazee juu ya miaka 60 wanatibiwa bure katika Hospitali za Serikali, Wakulima wanapewa ruzuku za pembejeo za kilimo, kwa mara ya kwanza CCM inajenga reli ya kisasa ya kimataifa itakayotumiwa ns treni ya umeme,  Mtandao wa barabara za lami umepanuka  hivyo sio jambo  la kiungwana kwa mtu kudai kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi

Ni ukweli kwamba  maendeleo ya mwanadamu hayana mwisho. Hata Tanzania ikifanikiwa kwa kiwango kikubwa kiasi gani, bado hayo hayatakua maendeleo ya mwisho, yaani maendeleo ya juu kabisa.

 Kila hatua katika maendeleo ya mwanadamu, huvutia hatua nyingine tena na huendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yetu ambapo hujitokeza vizazi vingine na kuendeleza pale tulipoishia.

Kutokana na msingi huo, ndio maana hata nchi zilizoendelea sana duniani, hazijawahi kufika mahali zikaridhika na maendeleo yake bali kila Siku Serikali zao zinajitahidi kupasua vichwa kuona ni vipi wafanye ili waweze kuendelea zaidi.

Ni jambo la wazi kuwa mambo mengi mazuri ambayo yana manufaa makubwa kwa taifa letu na yamefanywa na Chama Cha Mapinduzi hivyo kinafaa  kuungwa mkono na wananchi wote.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado hakijabadilisha asili ya kuanzishwa kwake ambayo ni kuwa chama cha kijamaa kinachojishughulisha na kutatua shida za watu na hivyo  kitaendelea kuweka juhudi ili kutatua kero  na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati husika na  kwa kulingana na mahitaji ya kipindi hiko.

Wasalaam,
Augustino Chiwinga.
0659438889.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages