Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akipongeza Katibu Mkuu mpya wa CCM Dk. Bashiru Ally baada ya kumteua na jina kupitishwa na NEC |
Kongole mwalimu Bashiri, haya niliyabashiri
Meng’ara kama nuru,yanini nibuguru?
Mejipa taknifu,umepata tahfif?
Kongole mwalimu bashiri,haya niliyabashiri
Umeng’ara kama Hariri,natena hakuna siri
Leo naweka wazi,naukata na mzizi
Hukuwa na inda mbaya,elimu kutupatia
Kongole mwalimu bashari,haya niliyabashiri
Matozi yanimwaika,nipo na babaika
Chuoni sitokuona, shairi ukighani
Shati la kitenge,ukiwa umelitenga
Kongole mwalimu Bashiri haya niliyabashiri.
Kijani utaivaa,chama kukitetea
Huna mtetemo,na elimu pia imo
Sera utatangaza,kule nahuku ukitangatanga
Kongole mwalimu Bashiri,haya niliyatabiri.
Chonde nakuhusia,shairi usilitupe
Nenda ukaghani,kutetea chako chama
Kapinge ufisadi,kwa miforasadi na ahadi
Kongole mwalimu bashiri,haya niliyabashiri
Tena usione soni,mafisadi kuwasonya
Chama kisikufie,nenda ukafyagie
Tena ukaghani,kwa shairi la shani
Kongole mwalimu Bashiri,hili nililibashiri,
Kalamu naweka tini,Hemed nainuka kitini
Titi la mama litamu,jingine halishi hamu
Arusha nimezaliwa ,jina nikaadhiniwa
Kongole mwalimu bashiri,hili nililibashiri
Hemed kivuyo
0655 250157
Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇