LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 14, 2018

RAIS MNANGAGWA WA ZIMBABWE AIMWAGIA SIFA TANZANIA


Victoria Falls, Zimbabwe
Rias wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (mwenye skafu) akiwa na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) wa CCM, Kanali mstafu Ngemela Lubinga (katikati mwenye miwani) na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe (anayemweleza jambo Rais Mnangagwa) pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa Zimbabwe Center for Democracy (ZCD) uliomalizika leo katika Hoteli ya Elephant Hills, Victoria Falls leo. 

Rais Mnangagwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ZANU-PF, alihudhuria mkutano huo na alitoa shukrani nyingi kwa ujumbe wa Tanzania kwa kuwapa elimu na uzoefu mzuri utakaowasaidia kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kwa amani na utulivu.

Ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ulijumuisha vyama vitatu vya siasa vya CCM, NCCR Mageuzi na ACT- Wazalendo.

Mhe Mnangagwa ni Rais wa pili wa Zimbabwe tangu wapate uhuru mwaka1980 kutoka kwa utawala wa walowezi. Pichani, Rais Mnangwaga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, baada ya kuufunga rasmi leo (14 MEI 2018) katika hoteli ya Elephant Hills, Victoria Falls, Zimbabwe.

Wazimbabwe wanategemea kufanya uchaguzi wao Mkuu baadaye mwaka huu (2018) ambapo Rais Mnangagwa anatarajiwa kupata ushindi  wa kishindo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages