Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe Dk. Obert Mpofu, Makao Makuu ya ZANU-PF Jijini Harare, jana. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amefanya ziara ya kukitembelea chama cha ZANU-PF cha nchini Zimbabwe ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa vyama hivyo kutembeleana ili kuimarisha na kuendeleza Uhusiano na Mshikamano wa kihistoria uliopo baina ya vya CCM na ZANU-PF, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa ZANU-PF. Katika ziara hiyo ameongozana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM Dk. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka na Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇