Mwenyekiti wa UWT Kabaka akizungumza leo |
Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) imetaka wateja sugu wanaodaiwa na Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kuhakikisha wanalipa marejesho ya mikopo yao mara moja vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Akizungumza katika Makao Makuu ya UWT Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Gaudensia Kabaka amesema UWT inaunga mkono Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya wanawake Tanzania (TWB) Beng'i Issa ya kutaka wadaiwa sugu wa benki hiyo walipe marejesho ya mikopo ndani ya siku saba.
" Sisi Umoja wa Wanawake Tanzania na wanawake wote wa Tanzania kwa ujumla wetu hatutakubali na hatuko tayari kabisa kuona watu wachache wakiwemo hata wanawake wenzetu wakitumia benki hii kwa kujinufaisha wao wenyewe". alisema.
Ameongeza kwamba UWT wanapenda kuona mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati ili wengine pia waendelee kukopa bila matatizo akisisitiza kuwa TWB ndiyo benki pekee inayoweza kunmkopesha mamam mjasiriamali mdogo na pia ni miongoni mwa benki tatu tu zilozopo duniani ambazo ni maalum kwa wajili ya wanawake tu benki hizo zipo Pakistan, India na Tanzania.
"UWT tunatoa rai kwa wakopaji wote na tunatoa tamko kwamba hao ambao wamekopeshwa na hawajarudisha mikopo kwa wakati wachukuliwe hatua za haraka na stahiki ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha wanalipa mikopo yao yote kwa manufaa na uhai wa benki yetu na kwa manufaa ya wanawake wote nchini.
Wadaiwa sugu ni 7065 ambao ni wengi sana hasa kutokana na fedha wanayoihodhi ambazo ni kiasi cha Sh. Bilioni 6.79. Tungependa kuona mikopo hii inarejeshwa kwa wakati" Alisema.
Alisema kuwepo kwa benki ya wanawake nchini ni maombi na kilio cha mda mrefu cha wanawake nchini tangu uhuru kupitia Jumuiya ya CCM kuzaliwa. ni kilio cha Kina bibi Titi Mohammed na mama Sophia Kawawa wakati wa uhao wao wakiwa wenyeviti wa UWT kwa nyakati tofauti na kilio cha wenyeviti wengine waliofuata hadi sasa.
"Napenda kuwaambia kuwa jambo hili Kama Mwenyekiti wa UWT nalifuatilia kwa karibu sana kwa kuwa ni miongoni mwa maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wetu, Rais Dk John Magufuli wakati wa Mkutano wetu Mkuu uliofanyika Desemba 8, 2017 mjini Dodoma", alisema
Alisema Uongozi mpya wa UWT umekaa na benki ya wanawake kuangalia namna gani benki itaweza kufikia wananwake wengi na kwa riba nafuu zaidi.
HABARI KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akifafanua zaidi kwa nini UWT ipo bega kwa bega na beki ya Wanawake Tanzania, wakat akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Baadhi ya maofisa wa UWT wakiwa kwenye kikao hicho
Waandishi wa habari wakimsikiliza Gaudensia Kabaka
Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi akifunga Mkutano huo na Waandishi wa Habari baada ya Mwenyekiti wake Gaudensia Kabaka (katikati) kumaliza kutoa taarifa nzito ya UWT. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara Eva Kihwelo Mwingizi.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇