DODOMA, Tanzania
Rais Dk.John Magufuli leo ameweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa awamu ya pili ya Reli ya Treni ya Umeme kutoka Morogoro-Dodoma-Makutupora katika eneo la Ihumwa, Manispaa ya Dodoma kwa kumtaka Mkandarasi Yapi Merzeki kutoka Uturuki kukamilisha ujenzi wa Reli hii ndani ya muda ili Watanzania waanze kuona manufaa ya Reli hii ambayo itasaidia katika kukuza Uchumi wa Nchi na kurahisisha sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania.
Rais Magufuli ameongeza kuwa Reli hii yenye gharama ya zaidi ya Tsh Trilioni 4 inajengwa kwa fedha za walipa kodi bila kupata ufadhili wowote na hivyo kutoa rai kwa Watanzania kulipa Kodi ili itumike kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.Wakati huo huo Rais Magufuli ameahidi ujenzi wa barabara ya lami kutoka barabara kuu ya Dar es salaam kuingia ndani eneo la Ihumwa.
Akimkaribisha Rais, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amemuhakikishia Mh Rais kwamba atasimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi CCM ili kuwaletea Watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na ujenzi wa Reli hii ya Kati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa TRC Ndg Massanja Kadogosa,kwa nyakati tofauti,wameelezea mradi huu wa Reli kama kati ya miradi michache inayotekelezwa Afrika na hivyo kuiweka Tanzania katika nchi zilizopiga hatua kubwa katika sekta ya Usafirishaji.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amempongeza Mh Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya maendeleo ambayo yanaigusa Dodoma kwa kiwango kikubwa na kuwataka wanaDodoma wachangamkie fursa za ujenzi wa Reli na maendeleo makubwa yanayotokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Your Ad Spot
Mar 14, 2018
Home
Unlabelled
RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UZINDUZI WA AWAMU YA II YA UJENZI WA RELI MOROGORO-DODOMA-MAKUTUPORA,AAHIDI KUJENGA LAMI IHUMWA-MANISPAA YA DODOMA
RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UZINDUZI WA AWAMU YA II YA UJENZI WA RELI MOROGORO-DODOMA-MAKUTUPORA,AAHIDI KUJENGA LAMI IHUMWA-MANISPAA YA DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇