* Wanavyuo wengi wageuza 'Google' kuwa Maktaba mbadala
* Watumia muda mwigi kuchati kutafuta na kuweka miadi na wapenzi
* Wakike waitumia kutafuta 'vibopa' wa kuwapa vitu vya thamani
Na Bashir Nkoromo
Matumizi mabaya ya Mawasiliano ya Inteneti ikiwemo mitandao ya kijamii kama facebook, Istagram yamesababisha kupatikana wasomi wengi wenye ufaulu wa juu kimasomo lakini wakiwa na uwezo mdogo wa uelewa wa fani walizosomea na hivyo kushindwa kumudu mazingira ya kazi baada ya kuhitimu vyuo.
Hali hiyo imeelezwa kuwa ni moja ya changamoto ambazo zimeonyesha kuanza kuwa kikwazo cha juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli katika kuwekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora nchini.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nashe (Pichani) wakati akizindua Program ya ' Uni Life Campus Program 2018' katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam. Program hiyo inalenga wanafunzi kujitambua.
Ole Nashe alisema matumizi mabaya ya Google ambayo hutumika kutafuta mambo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, yanadhoofisha mno uwezo wa mwanafunzi kudadisi na hatimaye kuwa tegemezi kiakili na kumfanya asipate maarifa na ujuzi uliokusudiwa na hivyo kushindwa mazingira ya kazi baada ya kuhitimu.
Alisema, wakati ili mwanafunzi ajenge vizuri uelewa wake kimasomo na kitaaluma lazima afanya tafiti zake kupitia kwenye Maktaba, wengi wa wanafunzi hawaende tena maktaba badala yake wamegeuza mitandao ya kijamii ndiyo maktaka zao jambo linalofanya tafiti zao zitokane na 'ku-copy na ku-paste'
Ole Nasha alisema kibaya zaidi, mitandao imekuwa ni uwanja wa kutafuta wapenzi na kuweka miadi za kufanya ngono kwa wanafunzi na ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili , kueneza propaganda na chuki pamoja na lugha mbaya kwa viongozi na watu wengine.
'Huu siyo utamaduni wa Kitanzania, hivyo nawataka wanafunzi kutumia Mitandao ya Kijamii kujitafutia maarifa na ujuzi utakaowasaidia sasa na baadaye.
Katika miaka ya hivi karibuni siasa na harakati vyuoni vimegeuzwa kuwa 'fashion' na hivyo kueneza siasa mbaya za kueneza vurugu ndani ya jamii. Vyama vya siasa vinawatumia wanafunzi kueneza siasa mbaya dhidi ya Serikali , Siasa za wanafunzi zinapaswa kuwa za kistaarab na zinazolenga maslahi yao kimasomo", alisema Ole Nasha.
Alisema wanafunzi wanaojiingiza kwenye siasa za vyama na uanaharakati hupungukiwa umakini wao kwenye masomo na hatimaye huishia kuingia kwenye mgogoro na vyombo vya sheria na baadhi yao kushindwa kumaliza vyuo hivyo ni lazima vyuo vyoye nchini kuendelea kusimamia vyema sheria za vyuo kikamilifu.
Ole Nasa alisema, tabia ya wanafunzi wengi hasa wa kike kupenda vitu vya anasa ambavyo hawana uwezo wa kununua ni changamoto katika kukwamia juhudi hizo za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini, kwani tabia hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa wasichana kuingia kwenye mahusiano na watu wengi wenye kipato kikubwa ili waweze kumudu gharama za kupata vitu hivyo vya anasa.
'Hali hii humlazimu mwanafunzi kutumia muda mwingi kuwafurahisha wafadhili hao na hivyo kukosa muda wa na umakini katika masomo, na vilevile inawazimu kutoa rushwa ya ngono kwa wahadhiri na wasaidizi ambao wengi wao ni wanafunzi wenzao ili waweze kufaulu bila ya wao kusoma, wanafunzi wa aina hii wakimaliza chuo huwa na ujuzi na maarifa kidogo kwa kuwa muda mwingi waliutumia kufanya mambo yaliyo nje ya masomo", alisema Ole Nasha.
Alisema ni kutokana na sababu hizo Program hiyo ya 'UNI LIFE CAMPUS PROGRAM 2018' ni muhimu sana ili kuwafanya wanafunzi na hasa watoto wa kike wajitambue na kuachana na tabia zinazoweza kuwaondoa kwenye mstari na kushindwa kufikia malengo yao.
"Serikali inaunga mkono Program hii, ili kuzipa nguvu zaidi juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli ambazo imekuwa ikichukua kwa hatua mbalimbali katika kuboresha Elimu kwa ujumla ili kutengeneza rasilimali watu itakayotoa mchango katika azima ya kujenga Uchumi wa kati na Viwanda", alisema Ole Nasha.
Alisema, katika juhudi hizo Seriakli imefanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kufundishia katika shule za Msingi, Sekondari na vyuo kama ukarabati wa wa shule kongwe nchini, Ujenzi wa Makktaba kubwa na ya kisasa yeneye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kufundishia ya Mlonganzila ambayo itaongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wa fani za afya na tiba kutoka 4,500 hadi kufikia 15,000.
Kugharamia mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ambapo katika bajeti ya mwaka 2017/18 kiasi cha sh. Bilioni 427.54 kiliinidhinshwa na katika robo ya kwanza jumla ya wanafunzi 119,435 wanaosoma ndani ya nchi na wanafunzi 351 wanaosoma nje ya nchi wamenufaika.
Pia serikali imeendelea kudhibiti ubora wa elimu ya juu ambapo kufuatia uhakiki uliofanyika jumla ya vyuo vikuu vitano, Vyuo Vikuu Vishiriki kumi, na Taasisi za Elimu ya Juu vinne vilifungiwa kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo wa 2017/2018 kwa kutokidhi viwango vya ubora.
Seriai imeendelea na utekelezaji wa Mpango wa Elimu-Msingi ambapo hutoa kiasi cha Sh. Bilioni 23 kila mwezi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wanafunzi hasa kutoka katika familia duni wanapata elimu bila kikwazo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇