LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 19, 2018

CCM YALETA FARAJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOPANDISHIWA KODI KIGOMA-UJIJI.

Na Augustine Chiwinga, Kgm
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa msemaji wake Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, kimeleta faraja kwa wafanyabiashara wa Kigoma-Ujiji  ambao Halmashauri ya Kigoma-Ujiji inayoongozwa na Chama cha ACT -Wazalendo ilikuwa imewabebesha mzigo mkubwa kwa kuwapandishia kodi ya vizimba kutoka Sh. 15, 000 hadi 
Sh. 50,000, tangu miezi minne iliyopita. 

Akiwa katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma tarehe 18/3/2018 Polepole alitangaza kufutwa kwa kodi hiyo mara moja akisema inaenda kinyume na Ilani ya CCM  inayozungumzia kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo na  inaenda kinyume na  misingi ya CCM ambayo ni haki na utu.

Polepole alisema, CCM ilielekeza Serikali  kuhusu kadhia hiyo  kisha Serikali ikatoa maamuzi ya kufutwa kwa ongezeko  hilo la  Sh. 50,000 kwa kizimba kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa imeonekana haikua haki na utu kwa wafanyabiashara hao kuongezewa kodi mara tatu zaidi ya kiwango cha awali cha Sh. 15,000.

Kauli hiyo iliibua furaha sio kwa wafanyabiashara tu bali hadi kwa wananchi wa kawaida ambao walikuwa wameathirika kwa kiasi kikubwa na ongezeko hilo kwa kuwa  wafanyabiashara  nao walikua wameongeza bei za bidhaa  ili kuwawezesha  kumudu kulipa gharama za vizimba.

"Hii ndio  CCM mpya inayoshughulika na shida za watu. CCM sikivu CCM inayowapenda, kuwathamini na kuwajali wanyonge wa Tanzania ni CCM iliyopania kuboresha maisha ya watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama", alisema Polepole. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages