Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo wakati alipofanya
ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlakaya
Kusimamia Uvuvi
wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John
Mapepele)
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye
suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi
Tanzania Bara Dk. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja
na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina
na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na
John Mapepele)
Baadhi ya watumishi
wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) wakimsikiliza
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka
hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. (Picha na John
Mapepele)
Kiongozi wa Kampuni
ya Linghang kutoka china inayoshughulika na uendelezaji
wa Utalii wa Zanzibar nchini china Tom Zhang (katikati) akiwa
na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji
wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John
Mapepele)
Na John Mapepele
Serikali imezipiga faini ya Sh. bilioni moja kila moja, meli 19 meli zilizotoroka bila kukaguliwa kwa mujibu wa sheria na zimetakiwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili.
Meli hizo ambazo kwa pamoja zitalipa faini ya jumla ya sh. Bilioni 19, zimepewa adhabu hiyo na Waziri Wa Mifungo na Uvuvi Luhaga Mpina kutokana na kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni ya kumi ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara au Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu zilizopo Fumba Kisiwani Unguja, Mpina amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Sh. Billioni moja kila moja zinatakiwa kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).
Aidha Mpina amesema meli hizo zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuiamru Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizo kuwajulisha kuhusiana na maamuzi hayo pia kuwajulisha Kamisheni ya Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia sheria kwa mujibu wa Sheria husika.
Aidha imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/ andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States (Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua. Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.
Wakati huo huo Waziri Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha 18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe 25/01/2018-27/01/2018.
Pia meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine ambao idadi yao ilikuwa mabaharia kumi.
Aidha meli hiyo pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.
Kutokana na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Sh. Billion moja ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG 1.
Mbali na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI XIANG 2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI XIANG 9 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.
Nyingine ni TAI XIANG 10 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI XIANG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/463, TAI HONG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN SHIJI 81 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN SHIJI 72 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/473.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Yohana Budeba amewataka wawekezaji kwenye bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia masharti na taratibu za kisheria ili nchi na wawekezaji waweze kunufaika.
“Taratibu zipo wazi ni muhimu kuzinangatia sheria namna nyingine tutaendelea kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye” Alisisitiza Dkt. Budeba.
Amesema hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzipiga faini meli hizo ni somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa yoyote atakayebainika kutenda makosa ya uvuvi haramu katika bahari na maziwani.
Aidha amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara na mtu yoyote ambaye atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.
Aliwashukuru wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa na wadau mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇