Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini
(220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa
shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Mahmoud Mgimwa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wanaofundisha katika kata ya Ihalimba katika jimbo la
Mufindi Kaskazini
Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini
(220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa
shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya
elimu na afya kwa wananchi.
Akizungumza na walimu wa kata hiyo
mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua
kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo
viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo
na kuendana na mazingira wanayoishi.
“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa
kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule
nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki
kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na
kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze
kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa
ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mgimwa
alieleza maeneo ambayo ametoa bati na mifuko ya saruji kuwa ni shule ya msingi Nundwe Bati
160 kwaajili ya nyumba ya walimu 60 na ukarabati wa paa la madarasa, bati 100. shule ya msingi Vikula
bati 100 na saruji 50, shule
ya msingi Mong'a bati 50,Zahanati ya Ugesa bati 30 na saruji 40
kwaajili ya nyumba ya mganga wa kijiji cha Wami, ujenzi wa nyumba ya mganga wa
kijiji cha Mbalwe bati 100 na saruji 20,Ihalimba sekondari nyumba ya mganga
bati 50 na fedha tshs 1,100,000 kwaajili ya dari jengo la maabara na kununua
pampu ya maji.
“Hizi ni gharama ni kata moja tu ya
Ihalimba ambazo nimezitafuta nako kujua mimi hivyo lazima walimu mjue kuwa kuwa
mbunge ni kazi kubwa sana na lengo la kuwa mbunge nikuhakikisha kuwa wananchi
wanapata maendeleo ambayo yanatakiwa kwa wakati sahihi hivyo napenda kuwapa
habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kata ya
Ihalimba kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa
Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba
wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta
maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo
wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.
Aidha
Mgimwa aliwataka walimu kumwambia changamoto ambazo
wanakumbana nazo ili kuzitatua na kuhakikisha walimu wanafundisha katika
mazingira mazuri.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Ihalimba
wilayani Mufindi mkoani Iringa Award Mahanga
amempongeza mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa kwa
kuendelea kutatua changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu kwa kuchangia saruji
mifuko 200 na bati 590 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule za
msingi na sekondari za kata hiyo.
Mahanga
aliesema kuwa mbunge Mgimwa amekuwa akijitoa kwa kutatua changamoto za wananchi
kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika.
Aidha Mahanga alisema kuwa mbunge huyo amechangia
kwenye sekta ya afya ambapo amefanikisha ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji
cha kata hii ya Ihalimba
Lakini pia Mahanga alimshukuru
mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa
kushirikiana na wananchi na kuahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi
anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneno
ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.
“Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa
akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa
wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo
nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Mahanga
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇