"Nimepokea kwa
mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu
zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na roli
katika barabara ya Nakuru Eldoret nchini Kenya.
Msiba huu
umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote
wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.
Kwa niaba ya
Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa
Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote
waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.
Naungana nanyi katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone
haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina".
Hizi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu katika Taarifa yake imemkariri Rais John Magufuli akisema wakati akitoa salamu za
rambirambi kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia ajali
ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu takribani 36 baada ya basi la abiria
kugongana na roli katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini humo leo tarehe 31
Desemba, 2017.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇