Aliyekuwa diwani wa kata ya Kwakilosa kupitia Chadema Joseph Lyata akionyesha barua ya kujiuzulu nafasi ya udiwani leo mbele ya wanahabari mjini Iringa |
Lyata akionyesha barua ya kujiuzulu kwake Udiwani |
Na MatukiodaimaBlog
KASI ya madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) jimbo la Iringa mjini kujiuzulu imezidi kuongezeka na kufikia madiwani sita sasa baada ya aliyekuwa diwani wa Kwakilosa Joseph Lyata na aliyekuwa diwani wa kata ya Ruaha Tandesy Sanga kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo .
Wakati Lyata akizungumza na wanahabari mkoa wa Iringa kujiuzulu kwake Tandesy Sanga amezungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam juu ya kujiuzulu kwake leo .
Akitangaza azma ya kujiuzulu kwake nafasi hiyo mbele ya waandishi wa habari Lyata amesema kuwa kujiuzulu kwake kumetokana na mahusiano mabaya ya kufifisha maendeleo kati yake na viongozi wa juu wa Chadema hicho akiwemo mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini pamoja na uongozi wa juu wa Chadema ukiongozwa na mwenyekiti wake Taifa Freeman Mbowe.
Lyata alisema kuwa mara kwa mara amekuwa akiandika barua kwa uongozi wa juu wa Chadema Taifa kuelezea malalamiko yake ya mahusiano mabaya kati yake na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa ila wamekuwa wakipuuza na kuwa hajaona sababu ya kuendelea kubaki ndani ya chama hicho japo safari yake ya siasa itaendelea kupitia chama chochote ikiwezekana hata CCM .
" Vyama vya siasa vipo vingi kuna CUF , ACT Wazalendo na CCM hivyo nitachagua ni chama gani kitanifaa kufanya siasa zangu ila hata CCM nipo tayari hakuna ubaya "
Alisema kuwa figisu figisu kati yake na mbunge Mchungaji Msigwa zilianza toka akiwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa na hofu ya mbunge Msigwa ni baada ya kuhisi kuwa anautafuta ubunge wa jimbo hilo mwaka 2020 .
" Mbunge alikwenda katika chombo kimoja wapo cha utangazaji mjini Iringa (Radio jina limehifadhiwa ) na kutangaza kuwa Lyata anautafuta ubunge kwa nguvu na hata wezi ila niwa wazi sioni kosa la kuzuiwa kugombea ubunge nikitaka na muda ukifika nitagombea ila namhakikishia kuwa sijaondoka katika Chadema kutokana na kununuliwa nimeondoka kutokana na mahusiano mabaya kati yangu na mbunge Mchungaji Msigwa na wapo wengi wanataraji kuondoka na kujiuzulu nafasi zao za udiwani " alisema Lyata
Kuwa mchakato wa kumpata naibu meya Manispaa ya Iringa nafasi ambayo alikuwa akiwania mbunge aliweza kuingilia mchakato huo na kupanga mtu ambae alimtaka na malalamiko yake alifikisha ngazi za juu ila walikaa kimya huku uongozi wa kanda kuptia katibu wake ulimpuuza kabisa na kuishia kusema kuwa ni msaliti .
" Uchaguzi mdogo wa udiwani Kimala Kilolo na Kitwiru mimi na Frank Nyalusi hatukupangwa kushiriki kampeni Kitwiru kwa hofu ya kutujenga kisiasa katika mbio za ubunge tulipangwa Kilolo ila kata yangu imepata maafa ya nyumba kuezuliwa mbunge hadi sasa pamoja na kuwa na taarifa hakuweza kufika aliyefika ni mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ambao waliweza kunisaidia hadi kuezeka nyumba za wananchi wangu ila mbunge badala ya kushukuru ameishia kunilaumu kuwa kwanini nimeezeka nyumba na pesa nimepata wapi "
Hata hivyo Lyata alisema kwa ajili ya kuonyesha ana nguvu ya kisiasa kuliko mbunge Mchungaji Msigwa ataendelea kufanya siasa na kuwa suala la ubunge 2020 asubiri muda ufike ila nyuma yake kuna kundi kubwa ya madiwani na viongozi wa chadema watakaomfuata bila kutaja majina na idadi yao alisema anaungwa mkono na madiwani hao kwa uamuzi wake .
Kuhusu tuhuma za kununuliwa na CCM kwa zaidi ya milioni 200 Lyata alisema hajanunuliwa na kama amenunuliwa basi ni mmoja mwa viongozi wenye sifa kuzidi ya hao wanaoeneza uvumi huu maana anayenunuliwa ni yule anayekubalika na aliyejiweka jikoni kama mmoja kati ya madiwani wa Chadema ambae amekuwa akieneza uvumi ila huku akitafuta kununuliwa na wana CCM
Kwa upande wake Edga Mgimwa aliyekuwa diwani wa Kihesa alisema kuwa amevutiwa na kujiuzulu kwa Lyata na kuwa katika mkakati wake wa kufanya kazi kama kada wa CCM jimbo la Iringa ni madiwani wengi watajiuzulu .
Mbali ya Lyata na Mgimwa madiwani wengine waliojiuzulu kwa mwaka jana na sasa ni aliyekuwa diwani wa kata ya Kitwiru kupitia Chadema Baraka Kimata ambae ni diwani tena wa kata hiyo kupitia CCM , pia wapo madiwani wa viti maalum wawili Husuna Ngasi na Leah Mleleu .
Mapema mwaka jana akizungumza na wanahabari mjini hapa juu ya kujiuzulu kwa madiwani wanne mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Mchungaji Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo hilo alisema kuwa kuna mkakati wa CCM kuendelea kununua madiwani na kukanusha malalamiko ya madiwani hao kuwa yeye ni chanzo cha wao kujiuzulu kwao .
Huku naibu meya wa Manispaa ya Iringa Dady Igogo alisema kuwa chama kimewanunulia vifaa maalum kwa ajili ya madiwani wa Chadema wanaonunuliwa kurekodi mazungumzo ya kununuliwa kwao .

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇