Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina
(mwenye miwani) baada ya kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha
Galinzila leo na kuongea na wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah
Chang’a (mwenye kofia) na kulia
zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
ya Ukerewe Frank Bahati leo. Mhe. Mpina
alichoma moto nyavu haramu za uvuvi
zenye thamani ya shilingi
bilioni mbili. (Na John Mapepele)
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia wavuvi
kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha
Galinzila Wilayani Ukerewe ambapo
baadaye alichoma moto nyavu haramu za
uvuvi zenye thamani ya shilingi
bilioni mbili katika kijiji
Kakukuru. (Na John Mapepele)
Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha
Galinzila wilayani
Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo
pichani) ambapo baadaye
alichoma
moto nyavu haramu za uvuvi zenye
thamani ya shilingi bilioni mbili
katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tano
ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo
(Na John Mapepele)
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe
Luhaga Mpina
ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi
bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika
visiwa vidogo
vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120
zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara
waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake
nje ya nchi.
Waziri
Mpina aliwaonya watu wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo
isiyoisha na kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua
stahiki za kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni
thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la
kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala yake
operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu
utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.
“Rasilimali zilizopo
ndani ya ziwa hili
ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya kuongoza kazi yetu ni
ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie ndio mtakaonufaika hivyo ni
itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha ulinzi, na mlinzi huyo akafanya
kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake alafu tajiri akamlalamikia kibarua
wake sisi na watendaji wa Serikali ni vibarua tu wenye mali ni ninyi
hatua tunazochukua zitaleta manufaa makubwa kwenu”alisema.
Pamoja na kuteketeza zana haramu, Waziri
Mpina alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa
Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti
wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita
50 ni asilimia 96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa
ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na
hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa
kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
“Tafsiri yake ni kwamba ziwa
halina samaki
wanaostahili kuvuliwa kulingana na kasi ya uvuvi na pia samaki
wazazi ni kidogo ambapo inatishia kumalizika kwa samaki na shughuli za uvuvi
kukoma katika Ziwa Victoria’alisema .
Akizungumza kwa nyakati tofauti na maelfu
ya wavuvi katika Visiwa vya Gagalini na Kakukuru wilayani Ukerewe Waziri
Mpina amesema hatua kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu
hazilengi kuwaonea wananchi wanyonge bali kuwatengenezea maisha bora ya kizazi
cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko
ziwani.
Akiwa katika eneo la Kakukuru
Waziri Mpina
alishiriki kuteketeza zana haramu zikiwemo vyavu za Makila 14,103, Kokoro 188 ,
Nyavu za dagaa 211, Nyavu za timba 450, Kamba za Kokoro 10,700 na ndoano
18,450 na Mitumbwi 109 zenye thamani ya sh. Bilioni
2.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwaidi Mlolwa amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kifungu cha 26 (i) (ii) kinamtaka kila mtanzania kulinda rasilimali
za nchi yetu ikiwemo samaki na mazao yake huku Sheria ya Uvuvi namba 22 ya
mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zikikataza vitendo vya kutumia zana
zisizoruhisiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,
Estomihn Chang'a alisema
Serikali ya wilaya
hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na
kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi
haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na
Mungu.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Ukerewe , Frank Bahati alisema halmashauri imewasimamisha
kazi watumishi watatu kwa tuhuma za kujihusisha na uvuvi
haramu.
Kwa
upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Waziri Mpina kuwasiliana na Waziri wa
Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ili kuona namna ya kudhibiti nyavu
zisizoruhusiwa kutengenezwa na kisha kuuziwa wavuvi.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇