LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 26, 2018

ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU TBC TIDO MHANDO AFIKISHWA KIZIMBANI

DAR ES SALAAM 
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. milioni 887 akiwa TBC.

Tido alifikishwa mahakamani leo saa 5:22 asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashitaka hayo matano.

Source: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages