Na Mwandishi Maalum,
Mkurugenzi wa
Mashtaka Bw. Biswalo Magaga, (DPP)
amesema , utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kutengenisha jukumu la
upepelezi na upelelezi mashataka umekuwa wa mafanikio makubwa
yakiwamo yakupunguza mlundikano wa
mahabusu.
Mkurugenzi wa
Mashtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akielezea utekelezaji wa mpango
huo tangu ulipoanzishwa kwa
sheria ya mfumo wa mashtaka
2007,mbele ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali linalokutana kwa
siku mbili mkoani Dodoma.
“ Tangu kuanza kwa
mpango huu tumepata mafanikio makubwa,
kwani kwa sasa kumekuwa na wafungwa
wengi kuliko mahabusu kwa maana kwamba
idadi ya mahabusu imezidi kwa 2000 kama
ilivyo kuwa huko nyuma ”. Akabainisha
Mkurugenzi wa Mashtaka.
Mpango wa serikali wa
kutenganisha shughuli za upelelezi na mashtaka
ulilenga kuondoa tatizo la haki
kuchelewa kutendekea na kesi kuchukua muda mrefu mahakamani kwa sababu ya muda
mrefu unaotumika katika upelelezi.
Mafanikio mengine kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ni jamii kurejesha imani kwa vyombo vya
sheria kutokana na haki kutendeka na kwa wakati na hivyo kupunguza vitendo vya wananchi kujichukulia hatua mkononi.
Mafanikio
mengine kesi zinazoendeshwa na
Mawakili wa Serikali zimekuwa na
mafanikio makubwa ikilinganishwa na zile ambazo
zinasimamiwa na mawakili
wakujitegemea. Kiasi cha kusababisha kupunfua kwa ukataji wa rufaa na mashauri ya jinani kupugua
kutokana na jamii kutambua uhalifu haulipi.
“ Kutokana na
utekelezaji wa mpango huu, siyo tu
kumepunguza rufani zinazopelekwa Mahakama ya
Rufaa kwa wakata rufaa
kupungua kutokana na weledi wa mawakili
na kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha serikali Mahakamani”.Amebainisha Mkurugenzi wa Mashtaka.
Akaongeza pia kwamba hata
barua za malalamiko kutoka kwa wananchi zimepungua kiasi kwamba mafaili hayajai tena barua za malalamikio kama ilivyokuwa
huko nyuma na hiki ni nikielelezo kikubwa kwamba wananchi wanapata
huduma za kisheria kwa ufanisi mkubwa” akasisitiza Mkurugenzi wa
Mashtaka.
Pamoja na mafanikio
hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka ameelezea baadhi ya changamoto
ni kutokuwapo kwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika baadhi
ya Wilaya hususani katika baadhi
ya Wilaya ambazo zinamtukio mengi ya jinai.
Amesema ufinyu wa
bajeti na upungufu wa raslimali watu
ndiyo unaochangia au kurudisha nyuma kasi ya ufunguzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kila
wilaya ili kuwafikishia huduma kwa karibu wananchi.
Katika hatua
nyingine, Mkurugenzi wa Mashtaka ametoa
rai kwa Mawakili Wafawidhi
pamoja na Mawakili wote kutekeleza majukumu yao ya kuisimamia Serikali bila woga na kwa kuzingatia maadili
na weledi na wasikubali kuyumbishwa.
“Tekelezeni majukumu
yenu kwa mujibu wa taaluma yenu, msiogope kusimamia ukweli na kile
mnachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yenu”. Akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇