Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Jana 30 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi, Jana 30 Disemba 2017.
Na Mathias Canal, Morogoro
Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, Jana 30 Disemba 2017 ametangaza KIAMA kwa
wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku
na serikali.
Amewataka
wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa
kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka
iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote
watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.
Ametoa agizo hilo akiwa
ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea Taasisi ya
Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Taasisi iliyopewa jukumu na
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la usajili wa wafanyabiashara wa
mbegu (Seed Dealers).
"Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu
jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi
matakwa ya wakulima wetu nchini" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Naibu Waziri huyo pia
ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kujitathmini kwa
utendaji duni kwani wameshindwa kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini
wafanyabiashara wanaokiuka maagizo ya serikali pamoja na taratibu na sheria za
nchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇