DAR
ES SALAAM
Watumishi
wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa
ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza
majukumu yake kwa ufanisi
Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na
Utalii jijini Dar es Salaam na aliyekuwa
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maendeleo
ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi.
Uzeeli Kiangi katika hafla fupi
iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa
mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika
nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.
Akizungumza
katika hafla hiyo alisema ‘’ Watumishi
ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza
majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’
Amesema
kupitia ushirikiano huo utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya
kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia
mwaka 2025
Aidha,
Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na
vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya
awamu ya tano haitawaacha salama.
‘’Wakati
wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu
anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza
majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza
Katika
hatua nyingine, Bi. Kiangi aliwataka watumishi wenye tabia ya kujituma kufanya kazi
pale tu wanapohisi kazi hiyo ina malipo wajirekebishe mara moja kwa kuanza
kufanya kazi zote zenye malipo na zisizo na malipo kwani zina umuhimu katika
kuwajenga kitaaluma.
Awali,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu alisema Idara yake
imejipanga kufanya kazi kwa kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo Mkurugenzi
Msaidizi, Bi. Kiangi aliyokuwa akiyapigania kwa ajili ya maendeleo ya utalii.
‘’Wizara
inatambua mchango wako tangu ulipoajiriwa mwaka 1984, tunakuahidi tutakutumia pale
tunapohitaji utaalamu wako ili kuhakikisha Wizara inafikia malengo
iliyojiwekea’’ alisisitiza
Kwa
upande wake, Afisa Utalii Mwandamizi, Josephat Msimbano wakati amesema Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa utumishi
wake alikuwa ni kiongozi aliyeichukia rushwa na yeyote aliyethubutu kutaka
kumhonga ili ahudumiwe kwa minajili ya kupindishwa kwa sheria aligonga mwamba.
Naye
Afisa Utalii, Domina Moshi amesema kwa
upande wake, Bi Uzeeli Kiangi alikuwa ni mshauri mzuri, alikua zaidi ya mama na
alipenda watumishi wajiendeleze kielimu na ndiye aliyemfanya aende masomoni
nchini kujiendeleza kielimu.
Bi.
Uzeeli Kiangi kastaafu kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma akiwa
ameihudumia Idara ya Utalii katika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33
ambapo aliajiriwa mwaka 1984 kama Afisa Utalii Daraja la tatu ambapo
alipandishwa madaraja hadi kufikia Afisa Utalii Mwandamizi daraja la kwanza
mwaka 2007.
Mwaka
huo huo alipandishwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Leseni na
Uthibiti kwa kipindi cha miaka mitano. Pia, mwaka 2013 hadi julai 2017 alikuwa
Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimpongezana na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia
Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika
Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa hafla fupi ya kustaafu kwake mapema mwezi Julai mwaka
huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia
Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika
Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka
huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Wakishuhudiwa na Afisa Utalii, Marygoreth Mushi (kwanza kulia)
na Mary Msekela (wa pili kulia)
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii,
Bi. Uzeeli Kiangi (kulia) akiwa na Afisa Utalii Mwandamizi, Martin Mrema
(katikati) wakiwa wanatabasamu huku
wameshika kwa pamoja moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi.
Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu
mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw.
Deograsius Mdamu
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii,
Bi. Uzeeli Kiangi (Kulia) akiwa na Afisa
Utalii Domina Moshi, wakiwa
wanatabasamu huku Bi. Kiangi akiwa
ameshika kwa moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha yake aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya
utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii,
Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa
Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya
Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi
akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake
1. Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia
Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika
Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati)
katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka
huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi
wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto) ( Picha zote na Lusungu Helela- MNRT)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇