Na Anitha Jonas WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini Koos Sibiya.
Mwakyembe ametoa wito huo jana jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.
“Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Dk.Mwakyembe.
Mwakyembe alisema atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini
Bondia Ibrahim Class aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.
“ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
Rais wa TPBC Chaurembo Palasea alisema mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi.
Your Ad Spot
Nov 13, 2017
Home
Unlabelled
MWAKYEMBE: WATANZANIA JITOKEZENI KUMSHANGILIA BONDIA IBRAHIMU CLASS
MWAKYEMBE: WATANZANIA JITOKEZENI KUMSHANGILIA BONDIA IBRAHIMU CLASS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇