Meza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman, Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani.
Bi. Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) akitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada za Diaspora katika sekta ya afya Zanzibar na kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa la Afya na kuwaasa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendeleza na kuthamini utamaduni wetu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇